HUYU NDIYE KWAME NKRUMAH
Mnamo mwaka 1935 ndani ya meli iliyokuwa ikitoka Pwani ya "Ghana" kuelekea Nigeria, alikuwepo kijana aliekuwa akifuata ndoto yake ya elimu. Jamaa huyo alikuwa Kwame Nkrumah.
KWAME NKRUMAH ALIZALIWA LINI?
21. September 1909 (Nkroful, Ghana) - 27. Aprili 1972 (Bukarest, Rumania).
Baada ya kufanya kazi ya kitaaluma nchini Marekani na Uingereza, Kwame Nkrumah alirejea nyumbani kuiongoza Ghana katika harakati za kutafuta uhuru na baadae kuwa rais wa kwanza nchini humo. Alishindwa hata hivyo kufanikisha dira lake la kuwa na Afrika kama nchi moja yenye mfumo sawa na wa Marekani.
KWAME NKRUMAH ALIJULIKANA KWA LIPI?
Kupigania umoja wa Afrika, kuiongoza Ghana katika kupata uhuru (1957) na kuwa Waziri Mkuu na Rais wa kwanza nchini humo (aliondoshwa madarakani kwa mapinduzi ya kijeshi 1966), kuunda Umoja wa Muungano wa Afrika (unaojulikana sasa kama Umoja wa Afrika).
ALIKOSOLEWA KWA MAMBO GANI?
Kuunga mkono falsafa za kijamaa, kujiita Marxist. Hili lilimpatia maadui ndani na nje ya nchi. Baadhi waliamini shirika la ujasusi la Marekani lilihusika katika kuondoshwa kwake madarakani.
KWAME NKRUMAH ALIHAMASISHWA NA NANI KATIKA MISIMAMO YAKE YA KISIASA?
Alijitumbukiza katika vuguvugu la ukombozi wa watu weusi wa Marekani, alikutana na Martin Luther King wakati akiwa Marekani, alisoma (na baadae kujadiliana na) mwanasosholojia, muumini wa umoja wa Afrika na mtetezi wa haki za binaadamu W.E.B Dubois. Wakati akiwa masomoni nchini Uingereza, alikutana na Waafrika wengi waliokuwa wakipigania uhuru wa Afrika, kama vile Jomo Kenyatta, Haile Selassie, Hastings Banda.
KWAME NKRUMAH ALIKUWA NA MISEMO GANI MAARUFU?
"Hatukabili Mashariki wala Magharibi: Tunasonga mbele."
"Mapinduzi yanaletwa na binadamu, wenye mawazo ya watu wa vitendo na wanaochukua hatua kama watu wenye fikra."
"Uhuru sio kitu ambacho binadamu mmoja anaweza kumtunukia binadamu mwengine kama zawadi. Uhuru lazima uudai kuwa ni wako na hamna mtu anayeweza kukuzuia."
Mwaka 2012, sanamu la Nkrumah lilizinduliwa katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, Ethiopia. Lakini kwanini Nkrumah? Nchini Ethiopia, wengi walihisi mfalme wao Haile Selassie ndiye anayestahili kutunukiwa cheo cha baba wa Umoja wa Afrika. Lakini Waziri Mkuu wa wakati huo wa Ethiopia Meles Zenawi, aliunga mkono kuchaguliwa Kwame Nkrumah.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?