Indira Priyadarshini Nehru Gandhi (Indira Gandhi)
19 November 1917 – 31 October 1984
Ni asubuhi saa tatu na dakika ishirini ya tarehe 31 Oktoba 1984, barabara ya Safdarjung, kwenye makazi yake, jijini New Delhi, alipokuwa akipitia bustanini kwake uku akitabasamu, na kwa mikono iliyoinuliwa na kukutanishwa kwa viwiko vya mikono yake, kama ilivyo salamu ya jadi na mila za Kiindi, akiwasalimia watu wake.
Alikuwa njiani akielekea kwenye kituo cha Runinga kwa ajili ya mahojino na mwigizaji wa toka Uingereza Peter Ustinov, ambaye alikuwa akipiga picha za filamu kwa ajili ya kituo cha televisheni ya Ireland.
Huyo hakuwa mwingine zaidi ya mwanamama na waziri mkuu pekee aliyewahi kutokea nchini India, akijulikana kwa jina la Indira Gandhi, na hiyo ndio ilikuwa siku yake ya mwisho duniani kutembea kwenye bustani hiyo.
Indira Priraadarshini Nehru alizaliwa tarehe 19 Novemba 1917 mjini Allahabad, kwenye Muungano wa Mikoa ya British India.
Mapema mwaka 1966, Indira Gandhi alichaguliwa kuwa Waziri Mkuu wa India akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Shastri. Ndani ya chama chake cha Congress, kulikuwa na kundi la viongozi wazoefu.
Waliamini kwamba wangeweza kuiendesha nchi, na Indira Gandhi abaki kama pambo tu hasa kwa kuwa ni mtu ambaye hakuwa na uzoefu mkubwa ndani ya chama na pia ati ni 'Mwanamke'.
Haikuwa hivyo, Indira Gandhi aligeuka na kuja na mipango mikubwa ili kujijengea Imani kwa wananchi. Mara kadhaa alitofautiana na wazee wa chama. Wakati fulani, kundi lenye ushawishi ndani ya Congress lilipeleka hoja kwenye kamati kuu kumfukuza uanachama Indira Gandhi ili apoteze nafasi ya Waziri Mkuu, lakini haikuwezekana.
Mwaka 1969, Indira Gandhi aliongoza sera ya kutaifisha Mabenki yote na taasisi binafsi za fedha zilizokuwa zinawanyonya wananchi.
Hili liliwakera zaidi baadhi ya viongozi ndani ya Congress kwani wallikuwa na Maslahi binafsi. Hivyo kukatokea mpasuko mkubwa ndani ya chama! Viongozi wazoefu wakijiita Congress Mfumo na upande wa pili Indira Gandhi alikuwa na damu changa za vijana.
Wakati wa uchaguzi mkuu wa 1971, Viongozi wazoefu ndani ya chama walipiga kampeni kumuondoa Indira Gandhi. Kampeni yao waliita "Indira Hatao" (Remove Indira) Ondoa Indira. Yeye alijua cha kufanya, haraka akaigeuza kuwa Garibi Hatao (Eradicate Poverty) yaani Ondoa Umasikini. Kwenye mikutano yote ya kampeni alisisitiza yeye sio tatizo, Bali tatizo ni Umasikini.
Kila aliposimama alisisitiza "Main kehti hoon garibi hatao, voh kehte hain Indira hatao" - (I say remove poverty, they say remove Indira) akimaanisha 'Nawaambia tuuondoe umasikini, wao wanasema Ondoa Indira' Ni kama utani vile, Indira Gandhi alishinda kwa kishindo kikubwa katika uchaguzi mkuu wa 1971.
Bila shaka yoyote aliutumia vema ule msemo kwamba adui zako wakikurushia mawe, Usiwarejeshee yaokote na ujijengee ngome madhubuti.
Mwaka 1975, Mahakama kuu ya Allahabad (Allahabad High Court) ilimkuta na hatia Waziri Mkuu Indira Gandhi kujihusisha na 'Michezo Michafu' wakati wa uchaguzi mkuu. Hivyo hukumu ilikuwa ni kumvua uwaziri mkuu.
Haraka alikata rufaa! Kabla haijasikilizwa. Akatangaza hali ya Hatari 'State of emergency' Hiyo ilipelekea kukamatwa kwa viongozi wa upinzani. Na kwa njia hiyo basi aliongoza mpaka mwaka 1977 alipoitisha Uchaguzi mkuu.
Muunganiko wa vyama vyote vya upinzani Janata Party Alliance ulimwangusha Indira Gandhi na kijana wake kipenzi Sanjay katika uchaguzi huu 1977. Morarji Desai akawa Waziri Mkuu.
Hapo ikawa ni kutukanwa kila sehemu. Kesi zikawa nyingi. Mara kadhaa alishinda mahakamani. Hakukata tamaa. Wengi waliamini ameisha kisiasa, lakini haikuwa hivyo!
Kukatokea mtafaruku ndani ya Janata Party, Wakati huo huo Indira Gandhi alikuwa na mahusiano mazuri na makundi mengi yaliyoipinga serikali. Uchaguzi mkuu wa 1980 alirudi kwa Kishindo na kuwa Waziri Mkuu kwa mara nyingine tena.
Pia chama chake cha Congress kilishinda viti vingi. Ni kama vile alijifunza kitu.
Indira Gandhi alifariki kwa kupigwa risasi na walinzi wake wawili, Satwant Singh na Beant Singh. Hii ilikuwa ni asubuhi ya Tarehe 31 Octoba 1984.
Alikuwa njiani akielekea kwenye kituo cha Runinga kwa ajili ya mahojino na mwigizaji wa toka Uingereza Peter Ustinov, ambaye alikuwa akipiga picha za filamu (Documentary) kwa ajili ya kituo cha televisheni ya Ireland.
Walinzi hao baada ya kumpiga risasi, wote wawili walizitupa silaha zao na Beant Singh akasema "Nimefanya kile nilichohitaji kufanya. Nawe umefanya kile ulichotaka kufanya."
Ndani ya dakika sita, Tarsem Singh Jamwal na Ram Saran, askari wa jeshi wa Indo-Tibetan, wakawakamata na kumuuwa Beant Singh. Na Satwant Singh alikamatwa na walinzi wengine wa Gandhi pamoja na kijana mwingine wakijaribu kutoroka, na Satwant Singh alijeruhiwa sana katika shambulio alililoanzishwa mwenyewe kwa ajili ya kujitetea asikamatwe.
Indira Gandhi alifariki wiki mbili na siku tano kabla ya kusherekea miaka 67 ya kuzaliwa kwake!
Satwant Singh alinyongwa hadi kufa mwaka 1989 pamoja na mshirika wake mwingine Kehar Singh.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?