Tuesday, 7 August 2018

 AVICENNA - IBN SINA

AVICENNA - IBN SINA - 1038th Birthday Mwanasayansi na Tabibu Bingwa Duniani In Google Doodle

AVICENNA (Abu Al Husein Ibn Abdullah Ibn Sina) alikuwa mwanasayansi mjuzi na mashuhuri zaidi katika falsafa ya elimu ya Utabibu wakati wa zama za kati (500 - 1450 AD).

Alijifunza hasa fani za mantiki, mitafizi kia (falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa), historia na utabibu. Ilithibitika thamani yake kubwa kama daktari pale alipoweza kumponya Prince Samanid aliyekuwa mgonjwa wa siku nyingi. Kama hidaya ya kazi yake hii kubwa, Ibn Sina aliruhusiwa kutumia maktaba ya kifalme ya Samanids ambayo ilimsaidia sana katika masomo yake. CHIMBUKO LAKE Wengi wangeamini kuwa historia ni shahidi wa michango mingi yenye manufaa ya Avicenna (Ibn Sina). Alishughulika kikamilifu katika vipengele vyote vya fani ya utabibu, unajimu, ushairi na taaluma ya uponyaji magonjwa ya akili. Elimu yake pana aliichangia kwa ustadi na uhodari katika matawi yote ya sayansi. Miongoni mwa kazi zake mashuhuri ni hivi vitabu vya "sanaa ya uganga" (utabibu) na "kanuni za utabibu". Ambapo kitabu cha kwanza ni Ensaikopidia ya kisayansi yenye kujumuisha Jiometri, Elimu nafsi (saikolojia), unajimu, Biothincs na muziki. Cha pili ni kitabu maarufu katika historia ya elimu ya utabibu (El-Kanun). Kitabu hiki chenye juzuu tano kilijumuisha kwa undani vipengele vyote vya fani ya utabibu mfano elimu ya Neurology na Saikolojia. Katika Nyurolojia yake Avicenna anatathmini ufichuaji na uponyaji wa hali kama upotezaji fahamu, uchovu, ukichaa, kifafa, majinamizi na ghamu. El Kanun ilizungumzia operesheni mifupa na mbinu za kutumia ganzi zinazohitajika kwa shughuli hizo, kama ukataji wa juu ya goti. Avicenna alitathmini tabia za aina arobaini za mimea zilizojumuisha njia za utoaji na utumiaji wa viini vya dawa (kutokana na mimea hiyo). Avicenna alikuwa mjuzi pia katika fani ya kusoma tabia za watu (Risal Aghlak) ambayo muono wa maadili wa Qur'an na sayansi ya Urazini imeegemea kwayo. Hii ni sehemu ya kipimo cha mitafizikia na anthrolojia ya kitabu kitukufu. MAFANIKIO Ukuu wa fanikio la kisayansi limepelekea maendeleo ya uchunguzi na majaribio. Fanikio hili ndilo msingi wa sayansi ya kileo. Yeye kama wanasayansi wenzake wa wakati wake, mfano Ibn Zuhr, Elkind, El Birun na Ibn Hafen alielewa miongozo ya Mtume Muhammad (saw) isemayo "Kutafuta elimu ni jukumu muhimu na la kwanza na kwamba wino (utumike kutafuta elimu) ni bora zaidi ya damu za watakatifu". Ibn Sina aliifafanua elimu ya utabibu kama stadi inayoshughulika kudumisha afya bora, kupigania dhidi ya maradhi na uponyaji. Mpango wa taifa wa afya umekuwa miaka minane katika kipindi chote cha zama za utabibu wa Kiislamu wakati wa Medieval na kabla ya kuanzishwa kwa mpango wa utunzaji afya katika Ulaya. Sayansi ya utabibu ya Kiislamu husisitiza elimu siha katika sehemu ya maisha ya mwanadamu ambayo bado ni muhimu na fasaha kwa zama zilizopita na maendeleo ya sasa. HITIMISHO Yatupasa kwa muda mwingi, kuthamini na kushukuru chimbuko la mwana falsafa huyu ambaye ni mashuhuri zaidi katika wanasayansi wa fani ya uganga.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!