Thursday, 26 March 2020


Je Ni Siraha ya Kibaiolojia,

Kwa Lengo La Kudhohofisha Uchumi wa Dunia?

TAHADHARI NA ONYO LA MWANDISHI.

TAFADHARI SANA USISHAWISHIKE NA UANDISHI HUU, MAONI HAYA SI LAZIMA YAAKISI UKWELI HALISI, HUU NI MTAZAMO TU NA FIKRA HURU ZA MTOA HOJA, USILAZIMISHE UKUBALIANE NAZO AU KUTOKUBALIANA NAZO.

Nadharia hii yaweza kukosa mashiko au kuwa dhaifu au kutokuwa na tija lakini kwenye siasa za ulimwengu si kitu cha ajabu na haswa wenye ajenda zao za siri katika harakati za kuitawala dunia.

VIRUSI VYA KORONA

kwenye tovuti za kijamii, kumekuwa na mijadara kadhaa, kuhusiana na virusi vya korona, na kumekuwa na nadharia nyingi zinasemwa kuhusiana na janga la virusi vya korona, kwanza tunapaswa kutambua kuwa virusi hivi si vigeni kwenye ulimwengu wa kibaiolojia... Vilikuwepo kabla na kuna aina zipatazo kama nne au tano za virusi vya korona.

Mpaka sasa kuna aina hizi za virusi vya Korona, vikiwemo vile vinavyo julikana kama SARS-CoV vya mwaka 2003, HCoV-NL63 (Human coronavirus NL63) mwaka 2004, HKU1 mwaka 2005, MERS-CoV mwaka 2012, na SARS-CoV-2 (zamani ilijulikana kama 2019-nCoV) mnamo 2019 inajulikana kwa jina la Covid19.

SARS (Severe Acute Respiratory Syndrome)
SARS-CoV 2003: Iliripotiwa kwa mara ya kwanza huko Asia mnamo Februari 2003. Ugonjwa huo ulienea kwa zaidi ya nchi 24 za Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Ulaya, na Asia kabla ya milipuko huo kudhibitiwa mwaka huo huo wa 2003.
Human Coronavirus NL63
HCoV-NL63: Coronavirus ya binadamu NL63 (HCoV-NL63) ni aina ya virusi vya korona ambavyo viligunduliwa mwishoni mwa 2004 kwa mtoto wa miezi saba nchini Uholanzi.
Human Coronavirus - HKU1
HKU1: Coronavirus ya binadamu HKU1 ni aina ya coronavirus ambayo ilitokana na panya walioambukizwa virusi. Na kwa binadamu, maambukizo husababisha ugonjwa wa kupumua na dalili za homa ya mafua ya kawaida, lakini inaweza kusababisha homa ya mapafu/yumonia (pneumonia) na Kikohozi. Virusi hivi viligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo Januari 2005 kwa wagonjwa wawili huko Hong Kong.
Middle East Respiratory Syndrome-Related Coronavirus
MERS-CoV: Virusi vya Korona vinavyo shambulia njia ya kupumua ya Mashariki ya Kati, au EMC / 2012, ni aina ya virus vya Korona ambavyo huwaambukiza wanadamu, popo, na ngamia.
SARS-CoV-2 ni jina la virusi ambavyo vimepelekea kupatikana kwa ugonjwa wa COVID-19. Ambao ndio unaotusumbua hivi sasa.

Mpaka sasa uelewa wetu wa wa "SARS-like coronavirus" (SARS-like CoV) ni kwamba ni kundi la virusi ambazo vinasaba vyake ni sawa na SARS-CoV lakini kundi hili hakijumuishi SARS-CoV au SARS-CoV-2. Kwa maneno mengine, SARS-related CoV = SARS-CoV + SARS-CoV-2 + SARS-like CoV.

Hivi ambavyo vinatusumbua sasa ni moja ya aina ya virusi ambavyo aidha vimefanyiwa modifikashen (Modification) au vimejifanyia Mabadiriko ya vinasaba (DNA mutation) vyenyewe kulingana na mazingira husika.

Kwa maana hiyo basi, tabia za Covid19 ni tofauti kidogo na virusi vingne vya korona, ambavyo kwa nchi za Arabuni vilishawahi kusumbua uko nyuma, ila hali haikuwa kama hii tunayohisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari.

Sasa basi, kutokana na mabadiriko ya kitabia ya virusi hivi vya korona, kumeibuka njama za kinadharia (conspiracy theory) kadhaa. na ukizisoma unaweza kushawishika na kuziamini, binafsi huwa sisumbuki au kuumiza kichwa kwa nadharia hizi. Kwa sababu hata zikiwa ni kweli au si kweli hazitanipatia furaha wala buraha zaidi ya uzuni na hasira tu. Sasa kuepuka hayo uwa ninapozisoma naziwacha tu kama zilivyo, na kuwaachia wapenda nadharia.


NADHARIA ZA KWENYE MITANDAO KUHUSIANA NA COVID-19

KUTOKA MAHABARA AU SOKONI? WUHAN - CHINA.
Kuna kitabu kilichoandikwa na Dean Kontz, kinaitwa The Eyes of Darkness, kwenye kitabu icho kilichotoka mwaka 1981, kinaeleza maambukizo ya Wuhan-400, vijidudu vilivyotengenezwa kwenye mahabara nchini China kwenye jimbo la Wuhan. Na vijidudu hivyo vimetengenezwa ili kutumika kama siraha za kibaiolojia.

Kwenye paragrafu moja kwenye kitabu icho kinatoa maelezo ya kina juu ya jinsi virusi vinavyoathiri mwili wa mwanadamu. Usahihi wa kushangaza ambao kitabu hiki cha 1981 kinatabiri kuzuka na kufanana kati ya 'Wuhan-400' na Coronavirus ni jambo la kushangaza kidogo.

Kwa wale watazamaji wa Netflix hivi karibuni wameachwa na mshangao kutoka kwenye tamthiria ya Kikorea inayoitwa Siri yangu Terrius (My Secret Terrius), ambayo ilionekana kutabiri janga la coronavirus Tamthiria hii ni ya mwaka 2018.

Watazamaji wengi wamevutiwa na sehemu ya mwisho ya safu ya kwanza, inayo ongozwa na waigizaji kadhaa nyota wa tamthiria hiyo kama vile So Ji-sub, Jung In-sun, Son Ho-jun na Im Se-mi.
Sehemu ya 10 ya tamthiria hiyo inaonyesha kuwa virusi vya korona, vimebadilishwa ili vitumiwe kama silaha, na uku madaktari wanaangaika kupata tiba yake.

UVUMI MKALI WASAMBAA DUNIANI
Mpaka sasa Wanasayansi hawajaweza kujuwa haswa asili ya COVID-19 lakini uvumi mkubwa ni kwamba virusi hivi vinatoka katika soko la vyakula, uko Wuhan au soko la samaki. Na hili kuwa uwenda virusi vilianzia kwenye soko la samaki, linaungwa mkono na ripoti kutoka kwa viongozi wa afya wa China na Shirika la Afya Ulimwenguni ambalo lilisema kwamba dalili zinaonyesha uwenda virusi hivi wameanzia hapo kwenye soko la samaki (Seafood Market), soko ambalo lilifungwa mnamo 1 Januari 2020.

Wakosoaji kwenye mabaraza ya mkondoni (online), hata hivyo, wamekuwa wakitoa tuhuma kwamba virusi hivi vinatoka mkoa wa Wuhan, kwenye Taasisi ya elimuvirusi (virolojia), maabara ya usalama ya Uchina ambayo inafanya utafiti na uainishaji wa kiwango cha juu cha virusi hatari zaidi.

UTHIBITI WA UCHUMI WA ULIMWENGU - CHINA au AMERIKA?

Yapo maneno mitandaoni/mkondoni ambayo yananasibisha na virusi hivi kuwa ni njia mojawapo inayochukuliwa na serikali hizi mbili, yaani serikali ya Amerika na serikali ya China, kudhibiti uchumi wa dunia na ikiwezekana kupunguza idadi ya watu duniani.

SERIKALI YA AMERIKA
Hapa kuna nadharia kinzani mbili, kuna ile ambayo inaeleza kwamba, Serikali ya Amerika imepandikiza virusi hivi uko China kwa lengo la kuwapunguzia nguvu ya kiuchumia Wachina, kutokana na kasi kubwa ya serikali ya China kwenye biashara ya viwanda duniani.

Na haya yametokea si kwa bahati mbaya, ila kwa malengo ya muda mrefu ambayo serikali ya Amerika ilikuwa haipendezwi na jinsi China ilivyoweza kutawala asilimia kubwa ya soko la bidhaa mbalimbali ambazo zina hatarisha uchumi wa Amerika na jamaa zake.

Lakini kwa akili ya kawaida, mtu anaweza kujiuliza, mbona hata Marekani nako kuna waathirika wengi tu wa Korona? Ni kweli wapo lakini kuwepo kwao kunatokana na aidha uharibifu kuelekea kwenye kujenga (Collateral damage) Uharibifu unaoweza sababisha vifo au uharibifu mwingine wa kiuchumi ambao ni matokeo yasiyotarajiwa ya oparesheni maalum.

SERIKALI YA CHINA
Wapo ambao wanailaumu serikali ya China kwa kutengeneza virusi hivi kwa malengo yao kadhaa, yakiwemo kudhibiti wale wote waipingao serikali ya China, haswa kisiwa cha Hong Kong.

Kumekuwepo sintofahamu ya muda mrefu kidogo, tangia jimbo la Hong Kong, kuachwa huru na Mwingereza tarehe 1 July 1997 na kukabidhiwa serikali ya China.

Kumekuwa na upinzani mkubwa kutoka Hong Kong, upinzania ambao unapelekea serikali ya China, kutafuta njia ya kuwanyamazisha wapinzani hao. Ndipo kukapelekea kufanyika kwa tafiti ambazo zinaweza kuwapumbaza wapinzani haswa wanaharakati wenye kutajika ambao ndio chanzo cha upinzani nchini China. Lengo ni kutengeneza virusi vitakavyo weza kupumbaza akili ya waathirika. Lakini kwa bahati ghafi, matokeo yamekuwa tofauti na matarajio.

LENGO CHINA NI KUITAWALA DUNIA KIUCHUMI
Nadharia nyingine ni la kiuchumi wa Ulimwengu, China imedhamiria kuitawala dunia kiuchumi na baadae hata kijeshi, ndio maana utaona China haijihusishi na migogoro ya kupigania au kugombanisha nchi ili kujifaidisha kiuchumi. Wao wapo zaidi katika kutoa mikopo ya fedha nyingi ambazo kwa nchi masikini si rahisi kuzirejesha. Hapo nchi husika inaposhindwa ndipo inajikuta inakabidhi njia zake za ucumi kwa serikali ya China kwa muda wa miaka kadhaa. Na serikali husika inajikuta haina maamuzi yoyote muhimu kwa mustakabari wa nchi zao na hapo ndipo nchi inapotawaliwa na nchi ya China.

Pili, China imeweza kusambaza virusi kwenye nchi kadhaa, lengo ni kuzifungia nchi hizo na matokeo yake uchumi wa nchi kadhaa haswa nchi tajiri, kutetereka na kujikuta wafanyabiashara wakubwa wa makampuni makubwa, kukosa mauzo na kupelekea soko la Hisa la kilimwengu, kushusha thamani ya Hisa. Na China kwa kuwa Uchumi wao ni Mzuri, basi Hisa hizo zinanunuliwa na China na sanjari na hayo, China inatangaza kudhibiti maambukizo ya virusi vya Korona uku nchi kadhaa za Ulaya na Amerika wanabakia wakiwa taabani kiuchumi wakisumbuka kutafuta kinga na ponyo.

Ndipo hapo sasa China itakapokuja na kutoa misaada kwa masharti kadhaa ya kiuchumia na kutoa dawa za kuponyesha au za kupunguza makali ya virusi na ikiwezekana kinga ya kila mwaka.

YAJUJ NA MAJUJ/GOG NA MAGOG.

Je Ndio Ushawishi wa Mashariki (Kikomunist) na Kimagharibi (Ubepari)?

Yajuj na Majuj/Gog na Magog
ni viumbe vilivyoelezwa kwenye vitabu vya dini ya Kiislam, Kiyahudi na Kikristo, kuwa siku za mwisho mwisho viumbe hao ndio wataiwala dunia kwenye kila kitu.
Wapo wanaofika mbali na kuhusisha nguvu hizi mbili za Kiuchumi, ambazo ni Ubepari wakiongozwa ma Marekani na baadhi ya mataifa ya Ulaya na Ukomonisti, ukiongozwa na Urusi na China.

Na ule ukuta ambao ulijengwa na Dhul-Qarnain kuwatenganisha Yajuj na Majuj, wananadharia wengine wanaunasibisha na ile hali mbili za kisiasa ya ulimwengu ambazo ni Ubepari na Ukomunist na ule ukuta ndio dhana ya Pazia la Chuma (Iron Curtain) kutenganisha dhana hizo mbili.

Mataifa yanayofata dhana mbili hizi zitafanikiwa kuvunja kuta, yaani zitaenea zaidi kuliko mipaka yao ya awali. Upanuzi huo unaweza kuwa wa kimantiki tu. Ikimaanisha kuwa itikadi zao (ukomunisti na ubepari) unaweza kuenezwa nje ya mipaka ya nchi zao.

Au itakuwa ni aina ya ukoloni yaani kukalia maeneo ya mashariki, Ulaya, Asia ya Kusini na maeneo mengineyo ya dunia. Au inaweza kumaanisha kuitawala dunia nzima.

Inafikiriwa kuwa baada ya kuteka ulimwengu, pia watakuwa na nguvu za kutuma vyombo anga za mbali (wataiteka mbingu)kwa maana ya kudhibiti anga na mawasiliano yote.

"Hivyo watatupa mishale yao kuelekea angani, na itawarejea zikiwa na alama kama za damu. Hivyo watasema: ‘Sisi tumekwishawateka wakazi wa dunia na tumewateka wakazi wa angani."

Ni dhahiri kuwa mishale inamaanisha Maroketi na vyombo vya angani kama satalaiti. Vyombo ambavyo vitarejesha taarifa mbalimbali za kiulimwengu. Zikiwemo taarifa kadha za watu, maeneo wanayoishi na hata wanako tembelea, maisha yao majumbani na makazini. Kutakuwa hakuna uhuru wala faragha binafsi, chochote utakachokifanya kitajulikana tu.

Na vyombo vingine vya anga vitaleta habari na ushaidi wa sayari zingine za mbali, hii inamaanisha kuwa vyombo vya angani vitafikia malengo yao na kurejea duniani vikiwa na taarifa ya kupendeza.
Kwa mujibu wa nadharia hii, wakati watakapokuwa wakijidai na kutakabari kuwa wameweza kugundua sayari uko anga za mbali, na wameweza kutawala kila kitu hapa duniani, kwa ufupi watakuwa wamefikia kilele cha mafanikio yao.

Ndipo watakapoletwa vijidudu vidogo sana ambavyo vitawaingia wanadamu kwa njia mbalimbali, na kuwaua. Hii inaonyesha kuwa hatima yao itakuwa kwa kuangamizwa kwa maafa magonjwa yasiosikia dawa, magonjwa ya kuambukizwa yatakayotokana na vijidudu vidogo sana (Virus).

ITAENDELEA...
---
TAHADHARI NA ONYO LA MWANDISHI LIZINGATIWE.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!