Friday, 17 July 2020

WAZANZIBAR KATIKA DIMBWI LA UKAFIRI.

Wa Sherehe za Mwaka Kogwa, Miji ya Unguja na Pemba.

Kama ilivyo miji iliyokuwa na Waislamu wengi na dini pia uwa na nguvu kiasi chake, Waislamu wa Zanzibar kwa miaka kadhaa iliyopita waliwahi kufikia hatua ya kufuata sharia chache katika Uislamu. Haswa zinazohusu ndoa na mirathi, na watawala (Sultani) wakiwateua makadhi kushughulikia hayo machache katika Uislamu.

Unguja Makadhi wa Kisunni ndio waliokuwa wengi na Pemba Makadhi wa Kiibadhi ndio waliokuwa wengi.

Licha ya mengi mazuri tunayo ambiwa na kuyasoma kwenye vitabu na vijarida, lakini Zanzibar nayo ina upande wapili wa imani, imani za Kikafiri, zilizojikita katika mioyo ya Wazanzibar kwa karne kadhaa sasa, kiasi baadhi ya mila zimekuwa ni ada kwao kuzitimiza.

Kila mwaka ifikapo kati ya mwezi wa saba na wa nane (Julai - Agosti) uko visiwani Zanzibar, kunakuwa na hekaheka za kusherehekea kukaribisha mwaka mpya wa Kikafiri, unaojulikana jina maarufu la Mwaka Kogwa.

ASILI YA MWAKA KOGWA

Hizi ni sherehe zenye asili ya Uajemi (Iran), na zinajulikana kwa jina la Nairuzi (Nowruz), yaani Mwaka Mpya wa Kiajemi au Siku mpya. Sherehe hizi zinatokana na dini ya Kimajusi (inayonasibishwa na dini za Uzorostani) waabudu moto na wanyama ya uko Iran.

Wenyeji hupenda kusema sherehe hizi zilianzishwa katika visiwa vya Zanzibar kutokana na mwingiliano wa kitamaduni kati ya wenyeji wa visiwa vya Zanzibar na Washirazi watu waliohamia wakitokea Iran, Ghuba ya Uajemi (Persian Gulf). Wakikimbia vita ambavyo vilitokana na uvamizi wa Waarabu Waislamu na kukimbilia Pwani ya Afrika ya Mashariki kati ya karne ya 6 au ya 7.

Washirazi si kwamba uko Zanzibar waliko kimbilia, walikuwa ni wageni, lahasha, bali Zanzibar ilikuwa ni moja ya vituo vyao vya kibiashara na uvuvi, tangia karne ya kwanza, 1BK.

Walipofika visiwani, waliwakuta na Wabantu na kuchanganyika nao, na visiwa vya Unguja na Pemba wakivihita ZANGBAR, Wakimaanisha Pwani au Ardhi ya watu weusi, wakifananisha na Zangbar, ya kwao Iran.

Mila na desturi zikachanganyika na baadhi kuendelezwa hadi leo hii, na tija yake ndio hizi sherehe za Mwaka Kogwa.

Mwaka Kogwa licha ya sherehe zingine mbalimbali, pia ujumuisha pamoja na kufanya ibada maalum za kikafiri (Moto) ikiwemo tambiko la kutambikia nchi ili kuleta bahati nzuri katika Mwaka Mpya.

Ibada ya tambiko, ufanywa na Mganga wa kienyeji, ambaye uwasha moto kibanda maalumu kilicho tayarishwa kwa ajili ya tambiko, uku anasoma dua, kwa kufuata mwelekeo wa moshi unapo elekea. Wakihitakidi kwamba mwelekeo wa moshi huo ndio wenye kutabiri mustakabari wa nchi aidha kuwe na kheri au shari kwa mwaka huo.

Baadhi ya michezo kwenye maadhimisho hayo ni pambano la kuchapana bakora, pambano ambalo hufanywa na wanaume tu, wanachapana kwa kila mmoja umchapa aliye jirani nae ili kutoana jeuri zao za mwaka uliopita. 
Zamani inasemekana zilitumika Silaha halisi lakini sasa hvi wanatumia fimbo zilizotokana na migomba, na aghalabu utokea vurugu kidogo za kuchapana kwa fujo.

Kiufupi Mwaka Kogwa ni sherehe ambazo, pamoja na mambo mengine, zinaashiria kuingia mwaka mpya wa Kiajemi (Nowruz).Tarehe hasa ya kuanzishwa kwa sherehe hizi haijulikani. Ila ni sherehe ambazo zimeshakuwepo kama sehemu ya mila za kale za wenyeji wa Zanzibar kwa zaidi ya mamia ya miaka sasa.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!