Saturday, 6 February 2021


HALI YA UBAGUZI UGHAIBUNI

Kwenye nchi hizi za Walami, kuna ufuatiliaji mzuri sana wa sheria za nchi na haswa haya masuhala ya kibaguzi au maneno ya kibaguzi.

Kumbagua mtu kwa namna yoyote ile ni kosa la uhalifu, jinai.

Maneno ya Kibaguzi yanaweza kuwa au kutona na:

Jinsia (Gender)
Kubaguliwa kutokana na jinsia yako.

Hali ya kimahusiano (Civil status – marital status)
Hali ya kimahusiano, au hali ya ndoa, ni uchaguzi wa mtu kwenye mahusiano ya mtu na mtu. Walioa, wasioolewa, waliopewa talaka na wajane ni mifano ya mingine kadhaa.

Hali ya Kifamilia (Family status)
“Hali ya familia” hufafanuliwa kama “hali ya kuwa katika mahusiano ya kifamilia kati ya mzazi na mtoto” Na ule uhusiano wa kuasili mtoto au watoto.

Umri (Age)
Kutobaguliwa kutokana na umri wako.

Asili (Race)
Hhii inajumuisha mwonekano wa rangi ya ngozi, kabila au utaifa.
Kutobaguliwa kutokana na rangi ya ngozi yako, kabila lako au utaifa wako, hii haijalishi kama wewe ni raia au mgeni ndani ya nchi.

Kuamini Dini au kuto amini dini (Religion or none)
Kumbagua mtu kutokana na imani yake ya kidini au kuto amini kwake dini yoyote ile.

Wakimbizi na wanaotafuta hifadhi (Refugees and Asylum Seekers)
Wakimbizi wa aina yoyote au wanaoomba ifadhi za kisias, awapaswi kubaguliwa kwa namna yoyote ile.

Ulemavu (Disability)
Kumbagua mtu kutokana na ulemavu wake

Mwelekeo wa kijinsia (Sexual orientation)
Mwelekeo wa kijinsia ni ile hali ya mtu kuwa na mvuto wa kimapenzi au wa kingono kwa watu wa jinsia tofauti au jinsia moja au jinsia zote.

Na mengineyo…

HALI HALISI YA UBAGUZI MITAANI
Mitaani kumejaa watu wa aina mbalimbali, wapo watu wenye mitazamo tofauti tofauti yenye kukinzana. Kuna wenye kupinga ubaguzi wa aina yoyote ile na kuna wachache ambao wao wanaona kuwa kuna baadhi ya watu (Haswa wale ambao hawana asili ya nchi ile) awapaswi kuwa na haki sawa na ikiwezekana wasiruhusiwe hata kufanya kazi, kiufupi warudishwe tu uko waliko toka.

Ukiwachunguza watu wa namna hii (Wabaguzi) ni kundi la watu waliokata tamaa na maisha yao na wengine wao wanahisi kuwa kutokana na kushindwa kwao kimaisha kunatokana na mwingiliano wa watu kutoka mataifa mengine.

Wapo wabaguzi wengine wanaona tu kuwa watu wa mataifa mengine haswa kutoka Afrika, India na Mataifa masikini ni watu wa kuwatumikisha tu kama watumwa na hawapaswi kuwa na haki kama wao.

Kwa hizi nchi za Yuropa, Wabaguzi wanabanwa na sheria za nchi na ni kosa la jinai.

Uzuri wa hizi nchi, ukifanya kosa lolote litakalo kufikisha Polisi au Mahakamani, basi kosa ilo linawekwa kwenye kumbukumbu zako…

Ikitokea umeomba kazi sehemu, basi utambue kabisa mwajili ataomba uthibitisho wa utihifu wako wa sheria za nchi na ataomba kupitia tovuti maalum ya polisi, uko atawapa namba yako ya Kitambulisho cha taifa (National Identification Number).

Polisi watachofanya ni kuangalia makosa ya jinai yaliyoko kwenye faili lako na kumfahamisha mwajili anayekusudia kukuajili. Mwajili akikuta kuwa una kesi au ulikuwa na kesi za kibaguzi au makosa mengine kuna hatari ya yeye kukunyima ajira na haswa makosa ya kiubaguzi.

Hii inapelekea wabaguzi wengi kuwa waangalifu sana wanapotamka au kutenda uhalifu wao, na haswa utokea pale ambapo wanahisi wakifanya ubaguzi hakuta kuwa na ushahidi au hata kama ushaidi utapatikana basi yeye kama yeye hana cha kupoteza na hata akishtakiwa. (HAw wengi wao uwa washa jichokea kimaisha).

MANENO KAMA HAYA UHESABIKA KUWA NI UBAGUZI
Ikitokea Mzungu (mtu yoyote yule) akimwita Mwafrika mweusi au mtu wa taifa lolote lile kwa namna hii, uhesabika ni ubaguzi wa rangi au utaifa:

“You black” au Akimwambia mtu wa taifa lingine “Go back to your country” au “Go back to your Cave” au akitamka N wods kama vile Nigger au Paki (ili utumika kuwaita Wahindi, pila kujali kama ni Mpakistani au lah).

Maneno yote hayo Mbele ya sheria ya nchi, yanahisabika kuwa ni maneno ya kibaguzi na ukimshtaki na ushaidi ukipatika atafungwa na hayo maneno yatawekwa kwenye kumbukumbu zake na athari yake ni kwa yeye kutopata ajira kwenye sehemu zenye kutoa uduma za kijamii na hata serikalini.

Na kama ni mwanasiasa au ni mfanyakazi wa serikalini basi yupo hatarini kupoteza ajira yake serikalini na hata kutopata nafsi ya kuongoza kisiasa.

Hali yoyote ya kiubaguzi Ikikukuta, usiogope kuwataarifu polisi au mashirika ya kutetea haki za binadamu, popote pale ulipo.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!