Monday 3 January 2022

 WATAWAAMINISHA NA MTAAMINI, 

KISHA MTAWAAMINI.

Hakuna Roho Mtakatifu Wala Mkamilifu Kwenye Siasa za Bongoland.

Sihasa, (ndio sijakosea ndio hivyo hivyo SIHASA) ni sawa na kurasa za kitabu, ukitaka kuijuwa usiangalie jarada lililo nje, unatakiwa ukifungue kitabu na kukisoma. 

Wengi wanafikiria kuwa wanaiujuwa siasa, kumbe wanacho kishabikia ni lile jarada lililowekwa nje ya kitabu, hawafungui wakasoma, tena ule usomaji wa kifasihi...

Juzi kati tumesikia mengi kuhusiana na kiongozi wetu moja mwenye shule yake, ambaye alituhamanisha kuwa kuna nyoka tena ni mwenye sumu kali, akatutaka wanafunzi wake tumuamini na kututaka tukamate magongo ili tuwe tayari kuuwa nyoka aliye hatari kutoka kwenye shimo lake.

Na sio huyo tu, tutawasikia wengine watakao jitokeza na wapo waliojitokeza, kisha tukawaona na kuwasikia wakajirudi, mfano wa yule msimamizi msemaji, wapo wengine wanatayarishwa.

Binafsi sina hofu na wabongo, kwa sababu nimeona wabongo ni kabila moja la ajabu na la kipekee sana duniani. Kwa kawaida watoto wote duniani wana nyongo. Ukiwafinya wanalia, ukiwatekenya wanacheka.

Lakini wabongo wao huwa hawana nyongo, hawajui kulia. Ukiwatekenya wanacheka, ukiwafinya wanacheka, ndio maana watu wanaweza kufanya lolote waliwezalo ili wapate wanayoyataka, hata kwa rafu, na wao wakahamaki lakini wakacheka tu.

Nakumbuka mambo haya yalianza tangia awali kabisa, wengi hawakujuwa yale maigizo ya tamthilia iliyopangwa na kupangika vyema kabisa, waigizaji wale walifanyiwa casting (Kuchagua Waigizaji Mahiri), yalianza mwaka 1995.

Aliletwa mmoja, akashangiliwa sana na hata misafara yake ilisindikizwa kwa kusukumwa na umma, wakajazana kwenye viwanja vya wazi, wakapewa matumaini na uku wakijazwa uvuvio wa hali ya juu, wakaamini kuwa huyo ni roho mkamilifu.

Matokeo tuliyashuhudia na tuliyaona.

Season ya pili 2000 ikafika kwa mbwembwe na shamra shamra, wenyewe wenye chama chao, wakamsimamisha yuleyule mtu wao, kwa sura na wajihi wake, hawakuitaji tena kuwapelekea bali waliona tu huyo anawatosha na kweli alitosha, maisha yakaendelea.

Season ya tatu, 2005 na ya nne 2010 na ya tano 2015 na ya sita 2020, season zote hizo, lile jungu kuu, lilijitahidi sana kupika na kuwaleta waigizaji mahiri, wataoweza kusajiriwa na upande wa pili, na ni kweli walifanikiwa sana, maana uko waliwapokea kwa nderemo na vifijo.

Wabongo ni viumbe wa ajabu kama nilivyosema hapo juu... Mfano ukiona mtoto anamwambia mtoto mwenzie kwa jambo la kitoto, watu wazima tutasema kuwa watoto wanacheza, na hata mtoto akimwambia baba yake kuwa gari ile ni langu au ndege ile ni yangu, baba hawezi sema kuwa wewe mtoto wacha uongo, atakacho sema baba ni kumtia moyo mtoto, kuwa ndege ile ikitua nitakuletea, huyu ni mtoto anakua. Lakini tunaposikia maneno ya kitoto anaambiwa mtu mzima, basi ujuwe hapo kuna walakini.

Ili tulilonalo sasa miezi hii michache ni dogo sana kuliko ilo linalokuja kwa sababu linalokuja tutakaa nalo si chini ya miaka kumi.

Lengo langu hapa ni kuwanasua wale wanaojiona kuwa wapo katika harakati za kidemokrasia zenye lengo la kuwapatia Watanzania wote fursa sawa wasije kuingia katika mtego huu, wakajikuta wanasajiri wale waliotengenezwa upande ule, maana maandalizi yake yamesha anza mapema mno.

Upande wa pili wamelala fofofoooo! 

Sasa ngoma iko wakati Wabongo wanapotaka kutafuta viongozi wao, pamoja na kuwa wote wanajua kuwa walioletwa ni waongo, hao ndio watabebwa na kumshangiliwa...


Neno ili “TUNGEJUWA” Siku zote huja mwisho wa safari... Na Majuto ni Mjukuu, USIAHI Haita Faa Tena!

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!