MOYO WA NGURUWE WAPANDIKIZWA KWA BINADAMU
Katika hali iliyo washangaza wengi na hata wanasayansi na madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo, ni pale madaktari wa mjini Maryland, nchini Marekani, walipofanikiwa kupandikiza moyo wa Nguruwe kwa mgonjwa wa moyo wa muda mrefu.
Katika ulimwengu wa kitabibu ndio mara ya kwanza kwa mtu aliye na ugonjwa wa moyo kupata bahati ya upandikizaji wa moyo wa nguruwe uliobadilishwa vinasaba.
Mgonjwa huyo wa kiume mwenye umri wa miaka 57 kutoka Maryland, nchini Marekani anaendelea vyema tangia alipofanyiwa upasuaji huo mwanzoni mwa mwezi wa Januari mwaka 2022.
Moyo huo wa nguruwe uliotumika ni wa Nguruwe mwenye umri wa mwaka mmoja, ulibadilishwa vinasaba katika upasuaji wa kwanza wa aina yake wa kupandikiza, Chuo Kikuu cha Madawa cha Maryland kilisema katika taarifa ya habari Jumatatu.
David Bennett alikuwa na ugonjwa wa moyo kwa muda mrefu, na moyo wa nguruwe ndio ulikuwa "chaguo pekee linalopatikana kwa sasa," kulingana na toleo hilo. Bennett alichukuliwa kuwa hastahili kupandikizwa moyo wa kawaida au pampu ya moyo ya bandia baada ya ukaguzi wa rekodi zake za matibabu kuonyesha kwamba hatoweza kuishi kama watatumia njia zingine za kawaida.
"Ilikuwa ni kufa au kufanya upandikizaji huu. Nataka kuishi. Najua ni risasi kwenye giza, lakini ni chaguo langu la mwisho," Bennett alisema kabla ya upasuaji.
Shirika la Chakula na Madawa la nchini Marekani (FDA) lilitoa idhini ya dharura kwa upasuaji huo katika mkesha wa Mwaka Mpya Desemba 31 2021, na upasuaji huo ulifanyika Januari 7 2022 kuanzia saa 8:30 asubuhi hadi 5:30 jioni.
Kabla ya kufanyiwa upasuaji huo, madaktari bingwa waliweza kuziondoa Jeni tatu ambazo zinahusika na kukataliwa kwa viungo vya nguruwe na mifumo ya kinga ya binadamu ziliondolewa kutoka kwa nguruwe, na jeni moja ilitolewa ili kuzuia ukuaji wa tishu za moyo wa nguruwe. Jeni sita za binadamu zinazohusika na kukubalika kwa kinga ziliingizwa.
Madaktari wa Bennett wataendelea kumfuatilia mgonjwa wao kwa usimamizi wa karibu, ili kuona ikiwa upandikizaji huo unafanya kazi ili kuweza kujifunza zaidi na kama manufaa yatapatikana ili siku za mbele viungo kutoka kwenye mwili wa Nguruwe vitumike katika kuokoa maisha ya binadamu wanaokabiriwa na matatizo ya viungo mbalimbali vya ndani, vikiwemo, Moyo, Mapafu, Figo n.k.
Madaktari hao wataendelea kufuatilia zaidi hili kujuwa kama kutakuwa na matatizo mengine kama ya mfumo wa kinga au matatizo mengine ya kiafya.
"Hakuna mioyo ya kutosha kutoka kwa wafadhili (Donor) ili kukidhi orodha ndefu ya wagonjwa wanaosubiri upandikizwaji wa viungo," daktari wa upasuaji Dk. Bartley P. Griffith alisema katika taarifa. "Tunaendelea kwa tahadhari, lakini pia tuna matumaini kuwa upasuaji huu wa kwanza duniani utatoa chaguo jipya kwa wagonjwa katika siku zijazo."
Revivicor, kampuni ya dawa iliyoko Blacksburg, Virginia, ndip ilitoa moyo huo, kulingana na taarifa ya habari.
Jumla ya watu 106,657 nchini Marekani wako kwenye orodha ya kitaifa ya kusubiri kupandikiza, na watu 17 hufa kila siku wakisubiria, kulingana na tovuti ya organdonor.gov.
Mnamo Oktoba 2021, madaktari wa upasuaji walifanikiwa upandikizaji wa figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba kwa mwanamke huko New York.
Caplan alisema ni mapema sana kuita upandikizaji wa moyo kuwa na mafanikio. Tutaita ni mafanikio pale tu ikiwa Bennett atakuwa na hali nzuri ya kiafya kwa miezi kadhaa mbele, alisema. Lakini bado inawezekana kwamba anaweza kufa.
Source:
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?