LESENI na BIMA ya KUFANYA SIASA!
Yaani Nawaza Kisichowezekana
Nimejiuliza sana, nikajiuliza tena na tena, hivi kwa nini Watoa Huduma wote wanatakiwa wawe na vyeti vya kufuzu masomo yao, na kama haitoshi, pale wanapotaka kufanyakazi wanapaswa wawe na leseni.
Mfano Madaktari, Walimu, Mafundi wanatakiwa wawe na vyeti vya ufauru na pengine kutakiwa wawe na leseni, mfano Madereva wa vyombo vya usafiri nakadharika.
Kiufupi ukitaka kutoa uduma za kijamii unapaswa uwe na leseni.
Leseni inawakilishwa kile ambacho mtoa huduma kuwa amekubalika kisheria baada ya kukisomea na kufanyiwa usahili na akafauru vizuri, hapo ndipo uaminika kuwa anaweza kuwaudumia wananchi.
Sasa basi kama hao wote wanatakiwa kuwa na vyeti vyenye kuonyesha ufauru wao na hata wengine kutakiwa kuwa na leseni, basi na WANASIASA nao wawe na VYETI vya UFAURU na kisha waombe LESENIi ya kufanyia SIASA.
Wawe wamefauru vizuri masomo kadhaa kwa kiwango cha digrii, aidha wasomee Sayansi ya Siasa au Uchumi (Political Science au Economics) n.k.
Na si Masomo ya sanaa kama vile Uigizaji (Acting), maana hatutajuwa kama wanaigiza au wanasema kweli.
Tena kabla ya kuomba kuingia kwenye siasa watume maombi na maombi yao yakikubaliwa basi wapatiwe mitihani na kutakiwa wafauru kwa kiwango kizuri.
Na baada ya kufauru watafute leseni na kukata BIMA REJESHI ya Malipo kwa Wananchi kwa taadhari, hili wakituletea ya kuleta basi tuweze kuwawajibisha kwa kuwanyang'anya leseni na ile BIMA iweze kulipia kile walicho kiharibu.
Wakitupandishia pandisha ovyo bei ya bidhaa, wakatwe mishahara yao kwa kiwango kile kile cha upandishaji.
Wakipandisha bei ya bidhaa muhimu kwa asilimia 15, basi na mishahara yao nayo inakatwa kwa asilimia ile ile 15 waliyopandisha...!
Nimewaza tu...
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?