Monday 11 July 2022

NI AIBU KUBWA KWA VYAMA VYA UPINZANI

Nchi ya Sri Lanka Ilikuwa Inaongozwa na Muungano wa Vyama 17 Vya Kisiasa Sri Lanka People's Freedom Alliance (SLPFA)

Matukio hayo ya Jumamosi yalikuwa kilele cha miezi kadhaa ya maandamano dhidi ya serikali yaliyochochewa na mzozo wa kufirisika kiuchumi kwa taifaSri Lanka.

Uchumi wa nchi ya Sri Lanka umezorota kwa kiwango cha kutisha, Sri Lanka imekumbwa na uhaba wa bidhaa muhimu kwa miezi kadhaa, kukatika kwa umeme kwa muda mrefu na mfumuko wa bei uliokithiri baada ya kukosa fedha za kigeni za kuagiza mahitaji kutoka nje.

Sri Lanka ina akiba ya mafuta ya Petroli ya kutosheleza siku moja tu iliyosalia, waziri wa nishati anasema, huku usafiri wa umma ukisimama huku mzozo wa kiuchumi nchini humo ukizidi kuwa mbaya. 

Waziri wa nishati Kanchana Wijesekera mpaka kufikia Jumapili alisema kuwa akiba ya petroli ilikuwa takriban tani 4,000, chini ya matumizi ya siku moja, huku foleni za kutaka kununua mafuta zikiwa na urefu wa kilomita kadhaa.

Taifa limekumbwa na uhaba mkubwa wa fedha za Kigeni, na mpaka kufikia siku ya Jumapili serikali iliongeza muda wa kufungwa kwa shule kwa sababu hakuna mafuta ya kutosha kwa walimu na wazazi kuwapeleka watoto madarasani, huku vituo vingi vya kusukuma maji vikikosa mafuta kwa siku kadhaa.

Hii ni aibu kubwa sana kwa wanasiasa wa upinzani na si Sri Lanka peke yake, maana huu ni uwakilishi tosha kuonyesha kuwa vyama vya upinzani kwenye nchi nyingi bado ni tatizo.

Hali hii ndio mpaka kufikia mwishoni mwa wiki, tukashuhudia kwenye vyombo vya habari Maandamano makubwa kutoka nchini Sri Lanka, maandamano yaliyopelekea Rais wa nchi na waziri mkuu kujiuzuru.

Waandamanaji waliokuwa na hasira walivamia makaazi rasmi ya Rais na Waziri Mkuu wa Sri Lanka, baada ya kuwashinda nguvu walinzi na waliokuwa wakilinda makazi ya Rais Ikulu na baadae makazi binafsi ya Waziri mkuu kupelekea kuchomwa moto.

Vikosi vya usalama vilijaribu kuwatawanya umati mkubwa wa watu waliokuwa wamevamia Ikulu ya Rais jijini Colombo mapema siku hiyo, huku makumi ya watu wakijeruhiwa katika mapigano hayo.

Msemaji wa hospitali kuu ya Colombo amesema watu kadhaa wanapatiwa matibabu kutokana na majeraha ya risasi, pamoja na wengine 36 wakiwa na matatizo ya kupumua baada ya kuvuta hewa ya sumu iliyotokana na mabomu ya machozi.

Rais Gotabaya Rajapaksa anatarajiwa kujiuzulu siku ya Jumatano, huku Waziri Mkuu Ranil Wickremesinghe alituma ujumbe wa kujiuzulu Jumamosi lakini hakuthibitisha tarehe rasmi ya kuondoka.

Kujiuzulu huko kunaashiria ushindi mkubwa kwa waandamanaji, lakini mustakabali wa watu milioni 22 wa nchi hiyo haujulikani huku wakihangaika kutaka kununua bidhaa mbalimbali ambazo zimekuwa adimu.

Chama kilichoko madarakani ni Muungano wa Vyama 17 Vya Kisiasa Sri Lanka People's Freedom Alliance (SLPFA)

source: Kutoka vyanzo Kadhaa mitandaoni


0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!