Ingawa hadi anaondoka alikuwa ameshaingiza kundi kubwa la watu katika Nyumba aliyokuwa anawaita waingie, ni wengi ambao waliingia wenyewe bila kuitwa kwa mdomo wake. Swali la kujiuliza “ILIKWAJE WAKAINGIA!?”
Ilikuwa ni matokeo ya kusimama kwake usiku palipo pelekea miguu yake ivimbe sana hadi mkewe kumuuliza kwanini anapata tabu kiasi hicho wakati amesha samehewa dhambi zake zilizopita na zitakazokuja.
Licha ya upole wake, Ukweli wake na maneno yenye nasaha njema, akiwalingania bila ya kuwakashifu au kuwakejeri kwa kile wanacho kiamini. Vilevile ilikuwa
ni matokeo ya kupenda kuwasamehe, kulipiza jema kwa baya, kuwaombea dua na kuwapenda wale waliomkosea maana aliwaona kama hawajui wafanyalo na wanafanya hivyo kwa kuwa hawajajua uzito wa aliyokuwa akiwaeleza.
Haya na mengine mengi yalipelekea watu kutoka maeneo mbalimbali hata wale waliompiga vita kwenda kupiga goti kwake nao wakasema “Nasi pia tumekuja kuingia”.
Kwa kuwa wengi wetu haya hatunayo, na kwa kuwa tunaiga tabia za KIKAFIRI, hatuwaiti kwa NASAHA NJEMA, wale ambao tunawaona sio katika sisi, KEJERI, KASHFA, MATUSI ndio zimekuwa hoja zetu, kwa wale wote ambao tunawaona kuwa si katika madhehebu yetu, japokuwa sote tunajiona kuwa tuna haki miliki na hati hiyo inatupa nafasi ya kuwatukana, wale wote wasiokubaliana nasisi, hakika itakuwa ngumu sana kwa ambao bado hawajaingia nao kuingia au hata kurejea tu kwenye “UISLAMU” wa kweli ingawa milango ya kuingia muda wote ipo wazi. Lakini tunaizuiya kwa maneno yetu yasio na ADABU wala HISHMA.
Tusije siku ya Hisabu, tukajikuta tupo nje ya nyumba tuliodhania kuwa tunayo haki miliki, na wale ambao tukiwaona kuwa si wenzetu, Uislam wao sio huu wetu, ndio wakawa wenye hati miliki.
Makafiri wanajikusanya katika umoja wao, wanafanya kila wawezalo wakitumia media kama vile Luninga, Tovuti na aina mbalimbali za vyombo vya habari kuupiga vita UISLAM, kama haitoshi nasi tunao jiona tupo ndani, kila kukicha tunapigana vita na hatusemeshani, kisa tofauti za Kiimani.
Basi tujue tusipo jirekebisha, tusije kumlaumu yeyote, pale nyumba tunao iona kuwa imetuifadhi, siku ya siku Mwenyenyumba akatutoa nje bila ya kutupa notice, kwa kuwa hatukuwa wenye kuiheshimu nyumba aliyotuachia tuishi, zaidi ya kuibomoa na kuharibu.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?