Saturday, 16 July 2016

Hivi karibuni tumeshuhudia kupitia vyombo vya habari kuwa baadhi ya wanajeshi nchini Uturuki, walikuwa kwenye harakati za kuipindua serikali ya nchi ya Uturuki kiasi cha kusababisha vifo vya watu wasiopungua 265 wakiwemo wanajeshi na raiya pamoja na polisi 17.

Baadhi ya wanajeshi wakaenda kwenye vituo vya Runinga (TV station) na kuwalazimisha watangazaji kutangaza kuwa jeshi limepindua serikali.

Wanajeshi hao wachache walisahau kuwa mwaka 2014 Mwezi wa nane, kulifanyika uchaguzi wa Rais na aliyekuwa waziri mkuu Tayyip Erdogan alichaguliwa kwa asilimi 51.79% za kura zote zilizopigwa akifuatiwa na Ekmeleddin İhsanoglu aliyepata kura asilimia 38.44% na Selahattin Demirtas aliyepata kura asilimia 9.76%

Mfumo huu wa kuchagua rais na wawakilishi wa wananchi kwa kifupi Demokrasi ndio mfumo unakubalika na nchi zote za Ulaya ukiachia nchi nyingine kama za Afrika na bara la Asia.

Huu ni mfumo uliojengewa hoja na vyombo vya fedha duniani pamoja na mataifa makubwa ya nchi za Magharibi kama moja ya masharti ya nchi kukubalika kupata mikopo toka kwenye vyombo hivyo na misaada kutoka nchi za Magharibi.

Nchi nyingi zimekubali kubadilisha siasa zao na kufuata masharti ya Umoja wa Mataifa, ili waende sambamba na masharti ili wakubalike kimataifa, nchi mojawa iliyoingia kwenye mfumo huu ni nchi ya Uturuki.

Baada ya ushindi huo chama ambacho kilionekana kuwa kina msimamo wa Kiislamu akikutarajiwa kushinda ni iki chama cha  Justice and Development Party (AK Party au AKP) ambacho kinaongozwa na Rais wa sasa Tayyip Erdogan.

Kumekuwa na minongono mingi kwenye medani za kimataifa kuwa chama iki kinaonyesha misimamo haswa kwenye swala zima la kuegemea kwenye Uislamu.

Chama iki kupitia Rais wake kimeonyesha kupigania umagharibi na wapo mstari wa mbele kuwa na urafiki wa karibu na serikali ya Marekani na wanajitaidi waingie kwenye umoja wa nchi za Ulaya (EU) lakini wakati huo huo wameonyesha kwa uwazi kabisa kupinga vita vinavyoendelea hivi sasa nchi Syria na ndio nchi pekee ambayo inapokea wakimbizi bila masharti na inawasaidia wakimbizi wa Syria na kuwaunga mkono Wananchi wa Palestina katika harakati zao za Kintifada.

Wadukuzi wa siasa za kimataifa wanasema kuwa chama iki kina ajenda ya siri ya kurudisha himaya au dola ya Uthmaniyya (Ottoman Empire) yaani Khilafa iliyopotea.

Kama vyama vingine chama iki cha AK kimepitia vikwazo kadhaa wa kadhaa na haswa pale kilipopata kashfa kwa baadhi ya viongozi wake kujihusisha na Rushwa, kiasi cha kupelekea kuwaondoa baadhi ya viongozi madarakani, na baadae kupunguza nguvu ya mitandao ya kijamii kama vile upatikanaji wa Twitter na YouTube, hii ilitokea mwaka 2014. Vilevile serikali ya hiki chama kimepiga marufuku utoaji mimba na matumizi ya unywaji wa pombe adharani.

Licha ya tuhuma mbalimbali kuhusiana na chama hiki na kukiona kuwa kina mwelekeo wa Kiislamu zaidi, bado kiliweza kupata ushindi wa asilimia karibia 52% na kukiwezesha kuongoza nchi.

Si kila mtu alifurahia hali hii wakiwemo baadhi ya wanajeshi ambao kwa kiasi fulani inaonekana kama walipata ushawishi kutoka kwenye nchi zingine za Kimagharibi na ndio maana walipojitangazia kuwa wamepindua nchi, nchi za Magharibi takribani zote ikiwemo nchi ya Amerika walikaa kimya wakisikilizia mwisho wake.

Uko mitaani nako hali ilikuwa shwari, hali ilibadirika pale Rais Tayyip Erdogan alipotangaza kupitia Runinga akisema kuwa kitendo hicho kilikuwa ni kinyume cha sheria na katiba. Na akwataka wananchi watetee demokrasia walio ipigia kura na akaahidi kuwaadhibu wale wote waliohusika na uhaini huo.

Na misikiti nayo ikaleta adhana na kuwaambia watu watetee serikali na wasikubali mapinduzi yale ya kijeshi yafanikiwe.

Ndipo raiya wa Uturuki walipoitikia mwito wa Rais wao na adhana za misikitini wakajitokeza kwa mamia elfu na kuingia mitaani, uku wakipiga takbira, Allahu Akbar... Allahu Akbar... Allahu Akbar... La ilaha illallah, Mohamadar Rasul Allah... na wakasimama mbele ya magari ya kijeshi vikiwemo vifaru na magari mengine ya deraya. Hali hii ikapelekea kuzuia waasi wasiende mbele zaidi. 

Naam wananchi kweli waliitikia mwito na wale wote waliokuwa wanategemea mapinduzi yale ya kijeshi wameanguka na kushindwa.

Serikali imerejesha madaraka yake, wanajeshi waliohusika wameshikwa na nchi imerejea katika utulivu na amani.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!