Saturday, 13 May 2017

Tafakari sana kuhusu jambo hili!

Nakumbuka kisa kimoja kiliwahi kutokea kipindi ambacho nchi ya Ujerumani ilipokuwa imegawanyika mapande mawali. Yaani Ujerumani ya Mashariki na Ujerumani ya Magharibi.

Nchi hii moja ilikuwa imegawanywa kwa kutenganishwa na ukuta mkubwa sana. Na kufanya kuwe na Mashariki na Magharibi ya Berlin.

Siku moja, baadhi ya watu kutoka Berlin ya Mashariki walichukua lori la mizigo na kulijaza takataka na kisha zile takataka wakazitupia upande pili wa ukuta ambako ni Magharibi ya Berlin.

Watu waishio upande wa Magharibi ya Berlin nao wangefanya kitu kama icho, lakini wao badala yake walichukua lori la mizigo wakaweka vyakula vya aina mbalimbali kama vile vyakula vya kwenye makopo, mkate, maziwa, mayai n.k.
Wakavipanga vizuri vyakula vile kisha wakapeleka upande Ujerumani ya Mashariki (East Berlin).

Baada ya hapo wakabandika lebo juu ya vyakula vile, ikiwa inasomeka hivi:

"KILA MTU UTOA KILE ALICHO NACHO"

Je umejifunza nini kwenye kisa hiki!?

TAFAKARI YANGU:

Na huu ndio ukweli haswa wa maisha yetu kwenye jamii!
Kila mtu ndani ya nafsi yake anaweza tu kutoa kile alichonacho nafsini mwake kuipa jamii yake, cha weza kuwa ni chenye faida au kisicho na faida.

• Waweza kusambaza chuki au upendo!
• Waweza kuchochea vurugu au amani!
• Waweza kuiokoa jamii au ukaiangamiza!
• Unao uwezo wa kujenga au kuharibu kama si kubomoa!

Unaweza kutafakari katika maisha yako kama utapenda... 
Je kuna kitu ambacho umekitoa kwa jamii kiasi jami ikafaidika?
Au ulichokitoa kimeleta hasara kwenye jamii?
Kumbuka...

"KILA MTU UTOA KILE ALICHO NACHO"

Tafakari sana kuhusu jambo hili!

Toa kilicho bora kwa jamii yako, usiwe chanzo cha vurugu au maangamizi katika jamii.

QUR'AN SURA AL- BAQARA [2]:267
Enyi mlio amini! Toeni katika vile vizuri mlivyo vichuma, na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi. Wala msikusudie kutoa vilivyo vibaya, hali nyinyi wenyewe msinge vipokea ila ingekuwa mmefumba macho. Na jueni kwamba Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujitosha na Msifiwa.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!