Sunday, 10 September 2017

ANA, ANA ANADO NA SIASA ZA BONGO
...Tu Mahodari sana wa kuonyoosheana vidole

Nakumbuka miaka mingi nyuma utotoni kulikuwa na hii tabia miongoni wa watoto. Ikitokea mmoja kajamba na hakawa hajajulikani basi, utasikia mmoja kati ya wale watoto anatoa ushauri wa kuimba huu wimbo wa “ana ana anado kachanika basto...”  uku akinyoosha kidole kwenye kila neno...! Na Yule wa mwisho ambaye wimbo utamwishia, ndio muhusika wa kujamba kule.

Hali hii aina tofauti na siasa za Bongo, kwa sababu wabongo wengi wenye kushabikia siasa ni mahodari na ni wajuzi sana wa kupiga ramli na kuagua matatizo mbali mbali kwa mtindo huu huu wa ana ana anado na uku wakinyoosha mkono upande mmoja na si kama vile utoto, wale wa utotoni walinyoosha vidole kwa kila neno moja kwa mtu mmoja, wakiamini hiyo ndio haki na kwa yule ambaye mwimbo utakaye mwishia ndio muhusika.

Hali hii naifananisha na washabiki na wanasiasa mbalimbali hapa Bongo likitokea jambo tu, basi wao tayari washajua na kila mtu kwa upande wake kisha imba ana “...ana anado...” na kumjuwa muhusika na dhamira yake.

Tumekuwa mahodari sana kiasi hata hatutaki kusubiri vyombo husika kufanyakazi eti kisa matokeo yanaweza kuwa kinyume na utabiri wa “ana ana anado”.

Kwanini linapotokea jambo tunakuwa wepesi sana wa kutoa maamuzi, kwanini tunapenda kujifariji kwa vitu ambavyo hatuna uhakika navyo?

Huu ni ukosefu wa baleghe ya kiakili na ili ni janga la kwanza kabisa kwa vijana wengi wanaotumia mitandao ya kijamii!

Vipi majibu yakitoka tofauti na vile tunavyotarajia, sura mtazificha wapi?

Matusi, kashfa, dharau, kejeli na kebehi hivyo vyote havitatoa majibu ya matatizo zaidi ya kujiongezea msongo wa fikra na kutugawa wakati sote sisi ni wamoja na taifa letu ni moja, kabila zetu, dini zetu na hata vyama vyetu, visitumike kutugawa kitaifa na kupoteza uzalendo wetu kwa nchi yetu hii.

Au ndio tumeamua kwa makusudi kabisa kuzibemenda akili zetu na hatukubali mtu yoyote mwenye mawazo yanakwenda tofauti na yetu, kiasi cha kuwa vipofu wa akili kwa kushindwa kuona au kutambua kuwa binadamu tuna uwezo tofauti katika kuyakabili mambo mbalimbali katika jamii inayotuzunguka, kwanini tutukanane!?

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!