Friday, 8 September 2017

TUNDU LISSU NDANI YA NADHARIA YA UHAINI 
Conspiracy Theory

TAHADHARI NA ONYO LA MWANDISHI.Tafadhari sana usishawishike na uandishi huu, Maoni haya si lazima yaakisi ukweli halisi, huu ni mtazamo tu na fikra huru za mtoa hoja, usilazimishe ukubaliane nazo.

JARIBIO LILE, JE NI MKONO WA SERIKALI?

Wapenzi wengi wa Tundu Lissu wamekuwa na hii nadharia kuwa serikali inaweza kuwa imeusika na hizi njama za kutaka kuwanyamazisha wapinzani na haswa watu aina ya Tundu Lissu kwa kuwa tu wamekuwa wakisigana sana na serikali kiasi cha kusababisha kuingia kwenye matatizo na serikali

Lakini hata hivyo na kwa vyovyote vile uwezekano wa mkono wa serikali katika jaribio la kumuua Lissu, linakosa uhakika na nadhanaria hii inakosa uhalisia. Kwa sababu kama serikali ikitaka kumnyamazisha, basi zinaweza kutumika mbinu mwafaka na za siri zaidi kuliko kutumia tukio la mauwaji ya wazi, kiasi kama vile wanataka sifa au kujionyesha kwa watu.

Jaribio lile limekuwa kama linatafuta sifa na aina ile ya kupotezana ni mbinu zinazotumiwa Majambazi na wauza madawa ya kulevya kwa lengo la kupeleka taarifa kwa wahusika kuwa ukileta za kuleta yatakupata kama yaliompata huyu.

JARIBIO LILE, JE UONGOZI NDANI YA CHAMA

Chadema wapo kwenye mbio za urais mwaka 2020. Lissu amekwisha jitengenezea sifa na umaarufu ndani na nje ya chama chake.

Wapinzani wake wanamuona kuwa ni mtu hodari katika mambo ya sheria na uwasilishaji wa hoja. Aidha ndani ya bunge au kwenye mikutano ya adhara. Japokuwa yeye binafsi hajawahi kutamka kuwa atachukua form za kugombea urais, lakini wenye mitazamo yao wanamuona kuwa hayo yote anayo yafanya basi aidha anatafuta tiketi ya kuogombea uwenyekiti ndani ya chama au apatiwe nafasi ya kugombea urais mwaka 2020.

Na sio siri kama atajitokeza kuchukua form basi wafuasi wengi sana wa chadema watamuunga mkono, kwa sababu amekwisha kukubalika, na ilo linawafanya wale wenye kutaka uongozi wa juu wa chama au watakao taka kuchukua form za kugombea urais kuwa na nafasi finyu sana.

Nadharia hii yaweza kukosa mashiko au kuwa dhaifu au kutokuwa na tija lakini kwenye siasa si kitu cha ajabu na haswa wenye ajenda zao za siri kama wapo ndani ya chama chake.

Hata hivyo tunarudia tena swali lile lile kwenye dhana ya kwanza, kwanini wasifanye kwa kificho?

JARIBIO LILE, JE NI UHAINI WA SIRI

Hapa wanapatikana watu wenye uwezo aidha kisiasa au kipesa kwa maana ya wafanyabiashara kubwa kubwa ambao kwa namna moja au nyingie wanasiasa vigogo hao na wafanyabiashara hao huwa wanafaidika moja kwa moja na uwepo wa serikali husika.

Sio siri, awamu hii ya tano, imekuwa mwiba wenye sumu kali sana kwa wanasiasa/vigogo wenye kutaka kujinufaisha au waliokwisha jitengenezea mazingira ya kujinufaisha kutokana na udhaifu wa kiutendaji serikalini.

Sasa kwa kuwa hawana nafasi tena na wengi wao wamekwisha haribikiwa, watakachoweza kukifanya ni kutafuta machafuko ndani ya nchi, ili serikali iliyoko ikose mapenzi kwa wananchi na kupelekea kuporomoka.

Kitendo cha kumpiga risasi Lissu, kinaweza kuwa ni moja ya mbinu hiyo ya kuichafua serikali ya Rais Magufuli. Rais ambae tayari wapinzani wanamuona kuwa anawaonea na amenyima uhuru wa kusema na amewabana sana.

Pili hata wale wafanyabiashara ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakifaidika kwa namna moja au nyingine wamejikuta kuwa awamu hii, mambo yao mengi yamekwama kiasi cha kuwatia hasara, kitu ambacho wao wanakiona kama si haki yao kutodhurumu na mbaya zaidi walisha zoea kujichotea pesa kiulaini na kuishi kianasa.

KILIO CHA SIRI CHA WAHAINI WA SIRI

Mbinu hii ya kunyamazishana kwa uwazi na kutafuta kuonekana bila kificho, linaweza kuwa ni mbinu kwa wapinzani wa Magufuli kutafuta kuonewa huruma nje ya mipaka ya Tanzania, kwa kutaka kuonyesha kuwa upinzani ndani ya nchi, unanyamazishwa kwa nguvu ya mtutu wa bunduki, na yote hayo ni kutokana na hali halisi ya wapinzani ndani ya nchi, kwa sababu tayari wanaonekana kuwa hawapewi nafasi ya kujitutumua kama ilivyo zoeleka.

Kwa hali hiyo basi kuna uwezekano pia ya wale WAHAINI WA SIRI wakaitumia nafasi hii, ili kuitisha kilio cha dharura na kuonyesha ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi inayo ongozwa kimabavu.

TAHADHARI NA ONYO LA MWANDISHI LIZINGATIWE.

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!