KIRINGO ANAWAKLISHA
JAMII ILIYOKUFA KIMAADILI
Hivi karibuni kumezuka mashtaka na tuhuma za bwana mmoja kuwa ana tabia za kuwalawiti watoto wadogo.
Kwa mtu yoyote yule kwa vitendo hivi vichafu hawezi kukubaliana navyo, na kwa wale wenye kuweza kuchukua hatua za kisheria kwa hakika watarifikisha swala ili mikononi mwa sheria.
Lakini haya yote au jambo lolote lina chanzo chake, japo twaweza kukijua au kutokijuwa. Na chanzo chake ni ile dharau na kibri cha kuona kuwa Wazanzibar ni malaika waishio duniani na hawawezi kufanya machafu hata kidogo.
Nakumbuka niliwahi kusoma mitandaoni, ripoti ya Utafiti uliofanyika mwaka 2014 uko Zanzibar kuhusu Hali ya Liwati na Ushoga imeelezwa kuwa asilimia 25 ya wanawake wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile ama na waume zao au na wanaume wengine kama njia ya kukimbia kupata ujauzito na mambo mengine.
Takwimu hizo zilitolewa na Katibu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar kutoka wilaya ya magharibi, Sheikh Nassor Hamad Omar, wakati akiwasilisha ripoti ya awali ya utafiti wa kamati ya kupambana na vitendo vya liwati katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu, kwenye kongamano la vijana kuhusu Udhalilishaji wa Kijinsia na Mimba za Mapema.
Alisema takwimu hizo zimekusanywa kutokana na utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Maimamu (JUMAZA) katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.
Na sababu ya kufanya hivyo, ama wanawake hao wanaogopa kupata ujauzito hasa wale ambao bado hawajaolewa lakini wako kwenye mahusiano yasio rasmi (Ndoa) na hata wale walioko kwenye ndoa.
Aidha utafiti huo umegundua watoto wengi wenye umri wa kuanzia miaka 9 hadi 20, wanaingizwa katika vitendo viovu ikiwemo liwati na usagaji.
Leo ni miaka kadhaa tangia ripoti hiyo itolewe adharani mwaka 2014, japokuwa swala ili limekuwa likijulikana sana na kila mtu akiulizwa anajuwa kuwa miji ya Zanzibar maswala ya Liwati yapo, japo yanafungiwa macho.
Kama ilivyo kawaida ya Wazanzibar wengi, hata ili laweza kuwa limeletwa na Wabara, maana Zanzibar kila ovu limekuwa ni jambo ambalo asili yake ni Bara.
Wizi umetoka Bara, Ulevi umetoka Bara, Ushoga na Usagaji janga ili nalo asili yake itakuwa bara tu.
Hii tabia ya kurembea kila ovu kuwa asili yake Bara, imekuwa ni jambo la kawaida sana, siku ukisikia askari amepiga mtu au nyumba fulani imeingiliwa na mapolisi basi utasikia maneno tu... "Mijitu ya Bara hiyo".
Zanzibar si Pepo kiasi kusiwe na mambo yote hayo, ulevi, umalaya, wizi, ushoga na maovu mengine yote yalikuwepo tangia zama za Sultani na yanaendelea mpaka leo.
Hii tabia ya kukana (The Denial of Reality - Kukataa Ukweli wa mambo...!) na kuona kuwa mabinti, vijana na wazee wa Kizanzibar ni Malaika hawawezi kujiingiza kwenye maovu, matokeo yake ndio haya, kwa sababu wazazi wameshindwa wenyewe kuwalea
watoto wao kwenye maadili mema kwa visingizo tulivyo vitaja, na matokeo yake ndio haya...!
Basi Wazanzibar wasubiri tu sasa serikali yao, ipitishe kisheria ndoa za jinsia moja, maana ndicho kilichobakia sasa...!
Itakapofikia viongozi kujulikana kuwa ni mashoga na wasagaji, kisha wakafuatiwa na wanamuziki na watu wengine maarufu, hakuna kitakacho bakia zaidi ya sheria kupitishwa, tena itapitishwa kwa kishindo kweli kweli...
MwenyeziMungu atuepushie mbali...!
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?