Wednesday 27 April 2022

MIMBA ZA KWENYE MAABARA

ARTIFICIAL WOMB FOR HUMANS

  • Ni Tumbo la Uzazi la Kwanza la Bandia la Kuwaumbia Wanadamu.
  • Teknolojia ya Tumbo Bandia - Watoto wa Kwenye Chupa
  • Je kutaleta hali ya Kudhibiti idadi ya Watoto Watakao Zaliwa Duniani?
  • Je Kuna Athari Gani Zinazoweza Kutokea kwa Hao Watoto Watakao Zaliwa Kwenye Maabara?
  • Tabia na Maadili ya hao Watoto zitakuwa ni za Namna Gani?

Hayo ni baadhi ya maswali ambayo mtu yoyote mwenye akili zake timamu anaweza kujiuliza...

Wanasayansi wanaendelea kutafiti kisayansi kuhusu njia mpya ya uzazi itakaotumika kutengeneza mtoto kwenye chupa kupitia maabara bila kufuata njia za kawaida za uzazi zinazohusisha ubebaji wa mimba na kuzaa.

Njia hii inaenda mbali zaidi, kuliko inayotumika sasa, ambayo mwanamke anaweza kupandikizwa mbegu na kuzaa, bila kujamiiana.

Wanasayansi hao wanachokifanya sasa ni kutengeneza mfuko wa uzazi wa binadamu kwenye maabara kwa maana ya mashine ya ujauzito, wakiamini, matokeo ya utafiti huo yataokoa watoto wanaokufa kabla ya kuzalwa au kupatikana watoto wenye ulemavu.

Wanasayansi hao wanadai kuwa njia hiyo inalenga kujali hali na afya za wanawake wanaobeba ujauzito, wao wanaona kuwa wanawake wanatumia muda mwingi kulea ujauzito kiasi kupelekea kuathiri miili yao kabla na baada ya kujifungua.

Utafiti huu unaitwa kisayansi 'artificial womb', unaofanywa na wanasayansi mbalimbali duniani wakiwemo kutoka Chuo kikuu cha Oslo, Norway, Chuo Kikuu cha teknolojia Eindhoven cha Uholanzi , Chuo Kikuu cha Singapore, na Taasisi ya sayansi ya Weizmann nchini Israel.

MCHAKATO UMESHAANZA

Wanasayansi hao kwa sasa wapo mbioni kutengeneza mfumo unaofanana na yuterasi ya mwanadamu, lengo ni kufanya mfumo huweze kubeba na kutunza mtoto sawa na mfuko wa uzazi wa mwanadamu.

Kwa mujibu wa wanasayansi hao, hilo linawezekana kufanyika kwenye mashine za kawaida za joto (incubators).

Majaribio ya utafiti huo yamefanyika kwa wanyama kama vile kondoo na kufanikiwa.

Kinacho fanyika ni kuunganisha mirija miembamba sana kwenye kitovu na kufanikiwa kupitisha damu kipitia mirija hiyo, na hilo linatasaidia kupeleka hewa kwenye fetasi, bila kuhitajika kutumia mapafu kufanya hivyo', anasema Dr Mathew Kemp, mtafiti kutoka Chuo Kikuu cha Singapore.

Utafiti huo umejielekeza kusisimua mifumo ya uzazi kwa kutumia kompyuta itakayoendesha roboti maalumu yenye mfanano wa mfumo wa uzazi wa mwanadamu.

'Kwa mara ya kwanza mwaka 1979, mtoto wa kwanza wa kwenye chupa alipopatikana kwa njia ya upandikizaji ya In vitro fertilization au IVF, kuliibuka hoja nyingi, kwa hiyo ni kawaida ukisikia watu wanasema tunaenda mbali ni hatari, anasema Dr. Anna Smajdor kutoka Chuo Kikuu cha Oslo.

KURUTUBISHA YAI NA MANII KWENYE CHUPA MAALUM

In vitro fertilization ni mchakato wa utungisho wa mimba nje ya tumbo la uzazi ambapo yai huunganishwa na manii katika vitro (chupa). Mchakato huo unahusisha ufuatiliaji na kuchochea mchakato wa ovulatory ya mwanamke, kuondoa yai au ova kutoka kwenye ovari zake na kuruhusu manii kuzirutubisha katika njia ya chupa kwenye maabara.

SWALI KUBWA LA KUJIULIZA

Swali kubwa la kujiuliza ni hili: Je ni nani atakae kuwa mmiliki wa teknolojia hii ya kuumba binadamu nje ya mifumo ya kawaida ya uzazi? 

  • Nani atakayeidhibiti? 
  • Na je itakuwa maalumu kwa watu gani? 
  • Au watu wote tutalazimishwa kuitumia njia hii mpya?

Ingawa kuna maswali mengi ya kujiuliza na hoja mchanganyiko kuhusu hatua hii ya kuumbwa kwa binadamu maabara, watafiti wenyewe wanasema kwamba, upo uthibitisho mkubwa wenye faida kubwa zaidi kwa binadamu ya kufanya hivi kuliko hasara.

Watafiti hao wanakadiria kwamba mpaka kufikia mwaka 2030, watakua washaanza rasmi majaribio kwa binadamu, huku wakiendelea kuruhusu mijadala na Midahalo ya kuboresha adhma yao hiyo.


Je Una Maoni Gani Kuhusiana na Jambo Hili!?

Source: Kutoka vyanzo mbalimbali mitandaoni "Artificial Womb"


0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!