Monday, 4 July 2022

 

NEBULA, ULIMWENGU WA MBALI 
NJE YA ULIMWENGU WETU

NEBULA NI NINI?

Nebula ni wingu kubwa la vumbi na gesi linalochukua nafasi kati ya nyota na kufanya kazi kama kitalu cha kuzalisha au kuunda nyota mpya. Neno Nebula ni neno linalotokana na neno la Kilatini Nebula, linalomaanisha “Umande, Mvuke, Ukungu, Moshi, Vukuto lenye joto.” Nebulae (wingi wa Nebula) huundwa na vumbi, pamoja na element kadhaa kama vile hidrojeni na gesi zingine zenye ioni.

Hali hii hutokea aidha kupitia mawingu ya gesi baridi kati ya nyota na vumbi au kupitia matokeo ya supernova.

Kuna aina nyingi za Nebula, Nebula iliyo karibu na ulimwengu wetu huu kwa maana ya Dunia inaitwa Nebula ya Helix (Helix Nebula). Haya ni mabaki ya nyota inayokufa, inayokadiriwa kuwa sawa au kama Jua hili linalotuangazia. Umbali wake ni takriban miaka 694.7 ya mwanga kutoka Duniani.

Hili ufahamu vizuri na kukadiria umbali wake, angalia umbali wa mwanga wa Jua (Sun) ili kutufikia uchukuwa dakika nane (8) tu za mwanga, na Jua letu hili lipo umbali Kilomita milioni 152.1 na mwanga wake uchukuwa dakika nane tu.

Sasa kadiria umbali wa kutoka kwenye Nebula mpaka Duniani ni kilomita ngapi, ikiwa tu mwanga wa Jua utufikia baada kusafiri ya Kilomita milioni 152.1 kwa dakika nane. Je umbali wa wastani wa miaka mia saba (700) za mwanga ni sawa na kilomita ngapi!?

Hata ikitokea binadamu kuwa na uwezo wa kusafiri kwa kasi yam wanga, bado itatuchukua mika mia saba, kufika kwenye Nebula iliyo karibu na dunia yetu hii.

Nebula zingine zipo mbali sana kutoka dunia yetu, baadhi ya Nebula kama vile Nguzo za Uumbaji "Pillars of Creation" ni eneo kubwa la nyenzo za kutengeneza nyota zilizoko kwenye Eagle Nebula, takriban miaka elfu saba (7,000) ya mwanga kutoka duniani. Michirizi hii ya gesi na vumbi, iliyofanywa kuwa ya rangi na mionzi ya nyota nyangavu inayofuka ndani, ikawa kama Milky Way.

Rangi ya bluu kwenye picha ya "Nguzo za Uumbaji" inawakilisha oksijeni, rangi nyekundu ni salfa, na kijani inawakilisha nitrojeni na hidrojeni.

Nguzo hizo zimeng'arishwa na mwanga ulio mkali sana wa urujuanimno unaowaka kutoka kwenye kundi la nyota changa lililo nje ya fremu.

Upepo wa moto mkali kutoka kwenye nyota hizi unamomonyoa polepole minara ya gesi na vumbi.

Kwa umbali huo ulivyo mkubwa kiasi hicho kuna uwezekano hata hizo Nebula au baadhi ya Nyota zilizo mbali kuwa hazipo tena ulimwenguni uwenda zishapotea au zilishakufa maelfu ya miaka kama si miaka milioni iliyopita ila mwanga wake ndio unatufikia sisi kipindi hiki.

UONI WANGU TOKA KWENYE QUR'AN

Tunasoma kwenye Qur’an Suuratul Maa'rij 70:4

“Malaika na Roho hupanda kwendea kwake katika siku ambayo kadiri yake ni miaka khamsini elfu.”
“The angels and the Spirit ascend unto Him in a Day the measure whereof is (as) fifty thousand years”.

Malaika na Jibrili wanapanda kwenda kunako toka amri yake kwa siku ambayo urefu wake ni miaka khamsini elfu kwa mujibu wa hisabu ya miaka ya duniani.

Na kama tunavyo elewa kuwa Malaika wameumbwa kwa Nuru, kwa maana hiyo basi tunaweza kusema kwamba umbali wanao safiri hao Malaika kutoka uko waliko mpaka duniani ni miaka elfu Hamsini ya Mwanga (50,000 light years).

0 comments:

Post a Comment

Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!