JASUSI ALIYEITUMIKIA NAFASI YAKE VEMA
Augustino Lyatonga Mrema 1944 - 2022
Augustino
Lyatonga Mrema alizaliwa Desemba 31, 1944 katika kijiji cha Kilaracha huko
Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, kaskazini Mashariki mwa Tanzania.
Alisoma shule
ya msingi huko huko kijijini na baada mwaka 1968 alifanya mtihani wa sekondari
kidato cha nne iliyoandaliwa na chuo kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza.
Mrema alianza
kazi mwaka 1966-69 kama mwalimu akifundisha shule mbalimbali za mkoa wa
Kilimajaro, ilopofika mwaka 1972 na 1973 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa
Kata.
Mwanzoni mwa miaka
ya 70 alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi, kwenye chuo cha
siasa cha Kivukoni jijini Dar es Salaam na alichaguliwa kuwa mwalimu wa siasa
katika wilaya mbalimbali kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi na baadae kwenye
miaka ya 80 alipelekwa Bulgaria, huko alisoma masuhala ya sayansi ya Ustawi wa
jamii na Utawala.
Na akaja kuchaguliwa
kuwa Mwalimu wa Chuo kikuu cha usalama wa Taifa na mwaka 1982 hadi 1984 bwana
Mrema aliteuliwa kuwa Kaimu mkuu wa usalama wa Taifa kwa mkoa wa Dodoma, mwaka
1983 hadi 1984 na baadae aliteuliwa tena kuwa Katibu wa Kikosi cha Ulinzi na Usalama
makao makuu Dodoma.
Mrema alikuja
na kuhamasisha kuanzishwa kwa vikundi vya ulinzi wa jadi, nje ya mikoa ya
Shinyanga na Mwanza vilivyoundwa na wananchi, maarufu Sungunsungu.
Jina la
Sungusungu pamoja na asili yake ni vikundi vyao lilitokea katika jamii za
Wasukuma. Jina hilo la Sungusungu lilianza kupata umaarufu tangu miaka ya 1980
kati ya Wasukuma walioona matatizo ya wizi wa mifugo na ujambazi kwenye
barabara baada ya vita vya Kagera na kurudi kwa wanajeshi wengi nchini kutoka
Uganda.
Hata hivyo,
vikundi hivyo vya sungusungu mara kadhaa vilishutumiwa kwa kutumia nguvu kupita
kiasi na kujichukulia sheria mkononi kwa kuwatesa baadhi ya watuhumiwa wa
uhalifu.
Mwanzoni mwa
miaka ya 1990 mpaka 1994, kabla ya kupelekwa kwenye vyama vya siasa na kuwa
mmoja wa wagombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, alikuwa waziri
wa mambo ya ndani ya nchi katika serikali ya awamu ya pili ya Rais Ali Hassan
Mwinyi.
Na baadae
aliongezewa cheo cha Naibu waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo
kwenye Katiba ya nchi ili kumpa nguvu zaidi ya utendani.
Itakumbukwa pia
mwaka huo wa 1992 kulipotokea fujo za kuvunja Mabucha ya kuuza Nyma ya Nguruwe
na ndio mwaka ambao Augustine Mrema alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu
Waziri Mkuu.
Waislamu
wataukumbuka mwaka 1992 kwamba siku hiyo waliyolazimika kuvunja baadhi ya
mabucha ya Nguruwe, ilikuwa ni baada ya watoto wa Kiislamu kuhuziwa nyama ya
Nguruwe kwa makusudi.
Hatua hiyo
ilifikiwa baada ya Waislamu kutoa taarifa Serikalini, juu ya hatari na athari
ya uwepo wa mabucha ya Nguruwe katika makazi ya imani za watu mchanganyiko,
lakini Serikali ilipuuzia. Siku ambayo watoto wa Kiislamu walipouziwa nyama
hiyo, iliwalazimu Waislamu kuvunja mabucha hayo.
Ndipo Rais
Mwinyi kwa hofu akasema wale waliovunja mabucha ya nguruwe "nguvu za dola
ziwaangukie" na ndipo Mrema akiwa ndio Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamu
Waziri Mkuu, akalitimiza hilo kwa vitendo.
Ilipofika mwaka
1994 alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo
ya Vijana na Michezo, mabadiriko haya hayakumpendeza, ilimpelekea Mrema
kuhamaki akidai mabadiliko hayo yalilenga kumnyamazisha asiendelee kupamba na
rushwa na wizi wa mali ya umma, akitolea mfano wa dhahabu iliyokamatwa uwanja
wa ndege wa Dar es Salaam lakini wahusika hawakuchukuliwa hatua yoyote.
Mwaka 1992,
mwaka ambao utakumbukwa sana na wale wanaofuatilia siasa za vyama kisiasa, kwa
sababu ndio mwaka ambao vyama vya siasa viliruhusiwa rasmi nchini Tanzania
kutokana na shinikizo la nchi wahisani.
Hapo ndipo sasa
serikali ya Tanzania, ilipoamua kuwapa ruhusa majasusi maalum waliokubuhu
kwenye siasa kwenda kuanzisha vyama vya upinzani, hili ionekane kwamba nchi ya
Tanzania ina vyama huru vya kisiasa.
Augustino
Lyatonga Mrema kwenye macho ya raia alionekana kama ni mpiganaji wa kweli wa
wananchi, akajiunga rasmi kwenye kambi ya upinzani, wakapatikana na wengine
wengi tu kama kina Mabere Marando, Makongoro Nyerere, Doktari Masumbuko Lamwai,
Edwin Mtei, gavana wa zamani wa benki kuu ya Tanzania na aliyekuwa naibu wake
Mzee Bob Makani na hawa watatu yaani Edwin Mtei, Mzee Bob Makani na Brown
Ngilulupi ndio waasisi wa CHADEMA.
Mrema
alipojiunga na NCCR-Mageuz, mwaka 1995, alifanikwa sana kisiasa, maana alikoleza
moto wa siasa, na alifanikiwa kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia chama
hicho.
Katika uchaguzi
huo, Mrema alikuwa mshindani wa karibu wa mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM),
Benjamin William Mkapa, Mkapa alishinda uchaguzi huo wa Oktoba
29, kwa kunyakuwa asilimia 61.82 ya kura huku Mrema akiibuka wa pili kwa kupata
asilimia 27.77 ya kura zote.
Umaarufu wake
ilikiwezesha chama cha NCCCR- Mageuzi kunyakua viti 17 vya ubunge Tanzania
Bara. Kwa kipimo cha wakati huo hii ilikuwa idadi kubwa ya viti vya ubunge kwa
kuzingatia miaka mingi ya nchi kuwa katika mfumo wa chama kimoja.
Walikuwepo pia
wabunge wa majimbo matatu ya Tanzania Bara: Karatu, Rombo na Kigoma Mjini
kutoka CHADEMA, pamoja na wabunge zaidi ya 20 wa CUF kutoka Zanzibar.
Mara zote Mrema
alikuwa akijinadi na kujenga wasifu wake juu ya uwezo wa ufuatiliaji wa kazi
ikiwemo kuzuru maeneo tofauti kwa ghafla hata nyakati za usiku, na kupambana na rushwa, ufisadi, magendo na
ulanguzi wa mali.
Hata baada ya
kushindwa urais, Mrema aliendelea na harakati za kuchaguliwa kwani Novemba 1996
alichaguliwa kuwa mbunge wa Temeke mkoni Dar es Salaam katika uchaguzi mdogo,
baada ya Mahakama Kuu kutengua matokeo ya uchaguzi wa ubunge wa 1995 yaliyompa
ushindi Ally Ramadhan Kihiyo wa CCM kwa sababu za udanganyifu.
Baadaye Mrema
alikihama chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na Tanzania Labour Party (TLP).
Hatua hii ilikuwa baada ya mgogoro mkubwa wa kiuongozi ndani ya NCCR-Mageuzi
kiasi cha kukiyumbisha chama na kukosa wabunge kwa muda mrefu.
Mrema Aligombea
urais kupitia TLP mwaka 2000 na kushika nafasi ya tatu na mwaka 2005 alimaliza
wa nne. Ni dhahiri kuwa matokeo hayo na idadi ya kura yalidhihirisha kushuka
kwa umaarufu wake kisiasa.
Kwa takriban
miaka 10 Mrema alikuwa Mwenyekiti wa bodi ya msamaha kwa wafungwa, maarufu bodi
ya Parole, mara ya mwisho aliteuliwa na Rais John Magufuli mwaka 2020.
Buriani, Mwendo umeumaliza Mzee Augustino Lyatonga Mrema.
0 comments:
Post a Comment
Je Una Nasaha zozote Kuhusiana na Makala hii?