Monday, 15 May 2023

 HIVI KWELI NILIKUFA AU NILIUWACHA TU UHAI KWA MUDA!?          Naamini Kabisa, Nilikufa Kwa Dakika Kadhaa, Ilikuwa ni Hali ya Kushangaza na Kustaajabisha Mno!      Ni Tukio Lililotokea Zaidi ya Miaka Kadhaa Nyuma, Kabla ya Mabasi ya Mwendokasi... Siku hiyo ilikuwa kama siku zingine tu zisizo na majina, ile hamu ya katembea kwa miguu na ile taswira ya jiji la Dar, ilisawiri barabara kwenye bongo...

Wednesday, 15 February 2023

TETEMEKO LA ARDHI NCHINI UTURUKI NA SYRIAKahramanmaras Lasababisha Watu Zaidi ya Elfu Ishirini na Nane Kufariki Dunia.Maisha ya Dunia sio Chochote Mbele ya Muumba na Yaweza Kukatika Ghafla Bila ya Kuletewa Taarifa. Tuna Amka Tukilala Tukiwa ni Wenye Kusindikiza Vijana kwa Wazee Kwenye Makazi ya Milele Wakipitia Ndani ya Barzakh.Zipo njia nyingi za kukatika maisha haya kama vile ajali, maradhi na mauaji. Hata hivyo, kuna aina nyingine ambayo kwa karne...

Monday, 6 February 2023

 GANDA LA HARAGWE KWENYE JINOHuku kazini, tulikuwa na mkutano wa kuongelea ufanisi utakaopelekea natija kwenye kazi zetu za Kila siku. Nilikuwa ni mtakadamu kwa siku ile, kwa wanao wasilisha mada...Kabla sijaingia kwenye chumba Cha mkutano, nikapitia maliwatoni, nikachua na udhu Ili nipate faradhi kabla ya mkutano kuanza. Wakati najiangalia kwenye kioo nikipaka mafuta kupunguza ukavu wa ngozi na baridi, wakati nafanya mkaguo, tahamaki...

Sunday, 8 January 2023

WAZIMU WA MADEREVA WA BODABODAHivi Waendesha Pikipiki Maarufu kwa Jina la Bodaboda, Bongo zao ni Zile za Zinjanthropus!?Safari ya Kutoka Kariakoo Mpaka Sinza, Kwa Siku Moja tu, Nilishuhudia Ajali Saba za Bodaboda. Nilipopata likizo yangu ya mwaka, nikafunga safari kwenda Bongo, baada ya kuondoka takriban miaka na miezi kadhaa, kwa kweli nilikuwa na hamu kubwa sana ya kukutana na ndugu, jamaa, marafiki na majirani zangu. Na haswa ukizingania...

Wednesday, 4 January 2023

MBIOMBIO NIKAJIKUTA NALIKIMBILIA GARI LA KUZOA TAKANilikutana Naye Kwa Kinyozi... Akauliza, Kwa Unyenyekevu Kabisa..!Basi bhana, Nipo Zangu Varandani, Mida ya Saa Tatu Hivi ya Asubuhi, Ghafala Huko Nje Nikasikia mlio wa Gari ya Kuzoa Takataka. Nikakumbuka Kuwa Nilipaswa Kutoa Pipa la Taka Tangia Jana Usiku... Nikakurupuka kama Swala aliyekoswa koswa na Simba.Mbiombio nikapitiza uwani, nikakutana na rasharasha za mvua, uku nikijikwaa kizingitini,...

Saturday, 24 December 2022

 WEWE UNGEFANYA NININA UNGEJISIKIAJE!?Hatoki Mtu Hapa... Mpaka Niupate...!Sikukuu hii, nilipata mwaliko toka kwa sahibu yangu mmoja, hayati ya ujana wetu tulikuwa wanagenzi katika moja ya shule ya awali, jijini Dar, Gerezani, Kariakoo.Sahibu yangu huyu imepita miaka mingi hatujaonana, kuonana kwetu ilikuwa kwa nasibu, wiki moja nyuma, nikiwa zangu kwenye harakati za hapa na pale, nikasikia sauti ya mtu anasalimia."Kakaa salamaa," akamalizia...

Monday, 5 December 2022

 NILIKWENDA KUNUNUA MWENYEWE DUKANIHivi Siku Hizi Bado Kuna Wanao Tafuna Tambuu!?Nipo Zangu Likizo, Ndani ya Jijila la Dar, Nakatiza Mitaa ya 'Uhindini' Karibu na Palipokuwa na Jumba la Sinema la Cameo, Lengo ni Kuelekea Walipokuwa Wakiishi Wakwe Zangu, Mtaa ya Kisutu.Nikaikumbuka hii mitaa enzi hizo nikiishi mtaa wa Livingstone, walikuwa wakiuza sana Tambuu, ila ni ayami sasa sijaona 'Wahindi' wala 'Waswahili' wakitafuna Tambuu.Zamani ukipita...

Friday, 2 December 2022

NILISHIKWA KWA TUHUMA ZA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA.Nilipo Ruhusiwa tu, Breki ya Kwanza Ilikuwa Maliwatoni...Nipo Ndani ya Ndege, Aina ya Airbus, Tumehabiri Watu Wengi Sana, Hii ni Moja Kati ya Ndege Kubwa Sana za Abiria, Ndege Inamilikiwa na Shirika la Ndege la Falme za Kiarabu la Imarati (Emirates).Nikitokea zangu ughaibuni moja kati ya nchi za Ulaya, naelekea zangu Afrika Mashariki kwa likizo fupi.Nitakaa Dubai kwa siku kama tatu hivi, kisha...

Tuesday, 29 November 2022

NILIKESHA NIKIMTAFUTATukio Linalo Fanana na Ukweli!Alhamdulillah Ndio Neno Nitakalo Lirudisha Kwa Mola Wangu Siku Zote Katika Uhai Wangu Ila Sintoweza Kumsahau Binaadamu Kwa Ukatili Wake...!Siku ya Jumanne majira ya saa mbili na nusu usiku nikiwa msikitini nikimalizia swala ya isha simu yangu ikiwa katika kimemeshi iliita mara nyingi sana, huwa sina kawaida ya kupaparika ninapokuwa mbele ya Mola wangu...!Alhamdulillah baada ya swala nilitazama simu...

Friday, 11 November 2022

 BIRIKA BATI, KIKOMBE BATI, NA HATUKUKOMA.Hivi wakulaumiwa walikuwa watengenezaji au wanunuaji au watumiaji!?Yaani hata sielewi, vikombe gani vinaunguza namna ile? Au walikuwa wanatukomesha tukivunja vikombe vya udongo!?Halafu kikombe cha chai, ila kinapicha ya nyanya. Sikuvipenda, sivipendi, sitavipenda.Na kwa nini nivipende, uwenda hivi vikombe ndio vimetukomaza midomo tukiwa bado makinda.Nahisi ndio maana Watanzania tumekuwa watu wa kupiga...

RAMADHAN KARIM

Read

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!